Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, March 24, 2016

Wakala wa pembejeo wilaya ya ulanga mkoani morogoro kutiwa mbaroni kwa tuhuma za rushwa.soma zaid.

Serikali wilayani Ulanga mkoani Morogoro
imeamuru kutiwa mbaroni kwa wakala wa
usambazaji wa Pembejeo,Novatus Naningwa na
wasaidizi wake pamoja na Afisa mtendaji wa
kata ya Kichangani na wa kijiji cha Kichangani
wilayani humo,wakituhumiwa kuwarubuni
wananchi kuchukua fedha badala ya vocha za
Pembejeo.
Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Christina Mndeme
amekiri kufikia uamuzi huo,baada ya wakala
huyo,wasaidizi wake na kiongozi wa kata ya
Kichangani na kijiji cha Kichangani kubainika
walikuwa wakiwarubuni wananchi kuchukua kiasi
cha shilingi 5000 ili wasaini wamepokea vocha
hizo za serikali ambazo nusu ya Gharama yake
imekuwa ikilipiwa na Serikali.
Amesema wakala huyo alipewa dhamana ya
kusambaza vocha hizo za Pembejeo katika kata
tatu za Kichangani,Lupiro na Milola,lakini yeye na
wasaidizi wake,Kuchungi Mussa, Ponsiasi
Chanja,Christopher Ponela na Rashid
Msasa,walishirikiana na mtendaji wa kata na wa
kijiji na kuwarubuni wananchi Wachukue
vocha,badala yake walisaini vocha Hizo na
kupewa shilingi 5,000 kwa kila mmoja.
Hata hivyo Amesema baada ya Uongozi wa
Wilaya kupata taarifa kutoka kwa raia Wema na
Diwani walimuandikia wakala huyo barua ya
kumsimamisha kuendelea na Huduma ingawa
aliendelea na zoezi hilo hivyo kuamuru
watuhumiwa hao watiwe mbaroni ili kufikishwa
mahakamani,huku Mtendaji wa kata na mtendaji
wa kijiji cha Kichangani wakikimbia na
wanaendelea kutafutwa.chanzo itv.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top