Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, March 24, 2016

Wafanyakazi 100 wa mgodi wa tanzanite waandamana kupinga kufukuzwa bila kulipwa mishahara yao.

Zaidi ya wafanyakazi mia moja wa mgodi wa
uchimbaji wa madini ya Tanzanite ya G and M
uliyopo katika Mji mdogo wa Mererani wilayani
Simanjiro Mkoani Manyara waliandamana hapo jana
kupinga hatua ya kampuni hiyo kuwaachisha kazi
bila kuwapa stahiki zao kwa kazi waliofanya kwa
zaidi ya miaka mitatu huku wakilazimishwa
kusaini mikataba mipya.
Wakizungumza kwa jazba wafanyakazi 
hao wamefanya kazi kwa zaidi ya miaka
mitatu na sasa wameachishwa ghafla kwani
walifika kwenye lango kuu la kuingia mgodini
wamekuta pamefungwa na kutakiwa wasiingie
ndani,wameiomba serikali iwasaidie kwakuwa
tayari wamiliki wameajiri wafanyakazi wengine na
wao kulazimishwa kusaini mikataba mipya.
Mwenyekiti wa wafanyakazi hao Adam Mosha
amesema hatua iliyo chukuliwa na uongozi wa
mgodi huo siyo ya kibinadamu na kamwe
hawatakubali kuacha haki yao.
ITV ilimtafuta Meneja wa Mgodi huo Elisante
Forcet ambaye amedai kuwa kampuni hiyo
haijawahi kuajiri wafanyakazi lakini huwa
wanawachukua kama vibarua na hivyo hakuna
mwenye haki ya kudai na kwa sasa kampuni
haina pesa za kuendelea kuwa na wafanyakazi
wengi kiasi hicho.chanzo itv.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top