Wilaya ya maswa mkoani shinyanga imepoteza milion500 kwa kumlipa mkandarasi hewa.
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Maswa
Mkoani Simiyu,imebaini kuwepo kwa matumizi
hewa ya zaidi ya shilingi Milioni 500,yaliyofanywa
na Meneja wa Mamlaka ya maji na usafi wa
mazingira Wilayani humo Mhandisi Jeremiah
Lema kwa Mkandarasi wa Kampuni ya Pett
Cooperation Ltd,anayejenga mradi wa chujio la
maji wa Zanzui bila kibali cha Bodi ya maji
Wilayani humo.
Mkuu wa wilaya ya Maswa Rosemary
Kirigini,ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo
amesema kuwa meneja huyo pia anadaiwa
kuidanganya kamati hiyo ya ulinzi na usalama
kuhusu ununuzi wa Krasha iliyodaiwa kuagizwa
toka nchini china
Mkurugenzi wa kampuni ya Petty Coopertion Ltd
inayotekeleza ujenzi wa mradi huo wa chujio la
maji wa Zanzui kwa ushirikiano na kampuni ya
Josam and Company Ltd Tryphon Elias,akatoa
ahadi ya kukamilisha mradi huo tarehe 30 mwezi
Mei.
Lugha gongana kati ya Mwenyekiti wa Bodi ya
maji wilayani Maswa Aloys Kimisha na Meneja
wake Mhandisi Jeremiah Lema kuhusu wananchi
kunyweshwa maji ambayo hayajatiwa
dawa,ikaibuka mbele ya Mkuu mpya wa Mkoa wa
Simiyu Antony Mtakaje, mkuu huyo wa Mkoa wa
Simiyu Antony Mtaka yuko tayari kuwajibika
iwapo wananchi wa Maswa watakunywa maji
yasiyotibiwa na kuugua magonjwa ya mlipuko
kikiwemo kipindupindu.chanzo itv tanzania.
0 comments :
Post a Comment