Breaking News
Loading...

Advert

Monday, March 21, 2016

Waziri wa TAMISEMI George simbachawene atoa tamko nzito kuhusu walimu wanaokataa kufundisha vijijini na kukimbilia mijini.soma zaid

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- TAMISEMI, George
Simbachawene ametangaza leo March 21, 2016
kuwashughulikia wale wote wanaofanya hujuma
katika sekta ya elimu nchini, wakiwemo Walimu
wanaokimbia sehemu zao za kazi hususani vijijini
na kukimbilia mijini.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari leo
March 21, 2016 alisema… ‘Katika eneo la upangaji
wa Walimu ni tatizo kubwa na nadiliki kusema
hadharani kwamba upangaji wa walimu kwenye
shule zetu ni wa ovyo leo hii tunaupungufu wa
ualimu kwenye vijiji kwa asilimia zaidi ya 40% na
ongezeko la walimu mijini ni kama asilimia 50%
kwa maana ya kwamba walimu wengi wapo Dar
es Salaam, walimu wengi wapo kwenye miji
mikubwa makao makuu ya mikoa na makao
makuu ya wilaya’ – George Simbachawene
‘Hata wanawake wanasema wanafuata wanaume
zao huko ni kukosa uzalendo kama ulikubali
kuajiliwa lazima ukubali kufanya kazi mahala
popote pale na watanzania ni wote mpaka
waliopo kule vijijini haiwezekani kukubali kazi
mjini na kukataa kijijini’ – George Simbachawene
itazame hii hapa video fupi.chanzo millard ayo.com

0 comments :

Post a Comment

Back To Top