Zaidi ya kaya 1800 hazina mahari pa kukaa baada ya mvua nyingi ikiambatana upepo mkali wilaya ya machame mkoani kilimanjaro.soma zaid.
Zaidi ya kaya 1800 katika kata ya
Machame Uroki, wilaya ya Hai Mkoani
Kilimanjaro zimekumbwa na maafa baada
ya mvua kubwa iliyoambatana na upepo
mkali kuezua mapaa ya nyumba, kungo’a
miti mikubwa na migomba iliyokuwa
inategemewa kwa chakula.
Wakizungumza kwa masikitiko wananchi
wa kijiji cha Uswaa wamesema mvua hiyo
iliyonyesha kwa muda wa nusu saa
imewaacha katika hali ngumu kimaisha
kutokana na mazao ya ndizi
yanayotegemewa kwa chakula na biashara
kuharibiwa vibaya.
Wananchi hao wamesema kuwa kutokana
na hali hiyo iliyotokea katika kata hiyo,
wako hatarini kukumbwa na baa la njaa
huku wazee wakisema mvua kama hiyo
iliyoambatana na upepo mkali iliwahi
kunyesha mwaka 1986.
Diwani wa kata ya Machame Uroki
Mh.Robson Kimaro amesema hali ya
wananchi siyo nzuri kwa kuwa upepo huo
pia umeathiri nyumba za ibada na
kwamba kata hiyo inahitaji msaada wa
chakula .
Kamati ya maafa ya wilaya ya Hai
imelazimika kutembelea kata hiyo na
kufanya tathmini ya madhara yaliyotokea
ambapo mkuu wa idara ya kilimo na
maafa amesema kwasasa wanatarajia
kuandaa taarifa ya awali na kuiwasilisha
ngazi za juu ili kuangalia uwezekano wa
kusaidia wananchi hao.chanzo jamii forums
0 comments :
Post a Comment