Aridhi ya mlemavu yapowra serengeti mkoani mara.soma zaidi.
Uongozi wa Serikali ya kijiji cha Ring’wani
wilayani Serengeti mkoani Mara, unadaiwa
kutumia nguvu kupora ardhi inayomilikiwa na
mkazi mmoja wa kijiji hicho kisha kuiza kwa
kikundi kimoja cha wachimbaji wadogo wa madini
kwa madai kuwa mmiliki wa ardhi hiyo ni
mlemavu na kwamba hana uwezo wa kuitumia
kikamilifu kwa shughuli za kilimo.
Akizungumza kwa uchungu huku akiungwa
mkono na baadhi ya wananchi wa kijiji hicho,
mkazi huyo wa kijiji cha Ring’wani Bw Emmanuel
Mataro,amesema licha ya kulima mazao
mbalimbali katika eneo hilo pamoja na ulemavu
wake,inasikitishwa kuona uongozi wa kijiji
ukimtaka kuondoka mara moja katika eneo hilo ili
likabidhiwe kwa kikundi hicho.
Naye Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha
Ring’wani kinacho tuhumiwa kupora ardhi hiyo na
kuiuza kwa kikundi kimoja cha wachimbaji wa
wadogo wa madini bila kushirikisha mkutano
mkuu wa kijiji Bw Masese Mgaya,amesema kuwa
serikali ya kijiji imetoa eneo hilo kwa agizo la
uongozi wa juu wa wilaya
hata hivyo akizungumza kwa njia ya simu Mkuu
wa Wilaya ya Serengeti Bw Ally Maftah
Mohamed,amesema ofisi yake haijawahi kutoa
waraka wa kumuondoa mwananchi huyo katika
ardhi yake kama inavyodaiwa na uongozi wa kijiji
hicho huku akitoa ahadi ya kufuatilia zaidi sakata
hilo.chanzo itv.
0 comments :
Post a Comment