Breaking News
Loading...

Advert

Friday, April 22, 2016

Donard Trump asalimu amri ahidi kubadilika.soma zaid.

Mgombea wa urais nchini Marekani kwa tiketi ya
chama cha Republican Donald Trump ameahidi
kubadilisha sifa zake katika mkutano wa faragha
na viongozi wa Republican.
Mfanyibishara huyo ambaye yuko kifua mbele
katika kuwania urais kupitia chama hicho alitoa
ujumbe wake kupitia wasaidizi wake ,kulingana
na chombo cha habari cha AP.
Kuimarika kwake katika mchujo huo kufikia sasa
kumekuwa na ishara miongoni mwa viongozi wa
chama hicho kwamba matamshi pamoja na sera
zake huenda zisiwavutie wapiga kura.
Majimbo matano yanapiga kura siku ya Jumanne
kumchagua mgombea wao wa urais.
Bwana Trump ana uongozi mkubwa wa idadi ya
wajumbe lakini huenda asipate wajumbe 1,237
anaohitaji kushinda mchujo huo bila ya mkutano
wa wanachama.
Wasaidizi wamewaambia viongozi wa chama
kwamba amekuwa akibadilisha sifa zake na
kwamba hatua hiyo imeanza kufua dafu.chanzo bbc swahil.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top