Breaking News
Loading...

Advert

Tuesday, April 26, 2016

Jeshi la polisi mkoani mbeya lapewa mtihani mgumu juu ya kukabiliana na ujambazi soma zaid.

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limeagizwa kutumia
nguvu na uwezo wake wote kuhakikisha
linapambana na kudhibiti ujambazi mkoani humo
ili wananchi waishi kwa amani na utulivu ambao
utawawezesha kufanya shughuli za kimaendeleo
bila hofu wala bughudha ya aina yoyote.
Mbele ya mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na
usalama ya mkoa wa Mbeya, ambaye pia ni
mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Gabriel Makalla
wakati akijiandaa kuzungumza na baraza la
askari wa mkoa wa Mbeya na baada ya wimbo
huo, kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya,
Justus Kamugisha akasoma taarifa ya jeshi hilo,
akieleza kuwa tangu kuanza kwa mwaka huu wa
2016 yametokea matukio mawili ya ujambazi wa
kutumia silaha.
Akizungumza na askari hao, mkuu wa mkoa wa
Mbeya, Amos Gabriel Makalla akatoa agizo kwa
jeshi hilo kutumia silaha za moto bila woga dhidi
ya majambazi watakaokuwa na silaha kama hizo.
Hata hivyo mkuu huyo wa mkoa akawataka
askari hao kuwa waaminifu na kusingatia maadili
ya kazi ya jeshi la polisi muda wote wa
utekelezaji wa majukumu yao.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top