Breaking News
Loading...

Advert

Tuesday, April 26, 2016

Sakata la Dr.Alex malasusa lachukua sura mpya.soma zaid.

Sakata la Malasusa, watoto watoroshwa
MUME wa mwanamke anayedaiwa kumkamata
ugoni Askofu Dk Alex Malasusa wa Kanisa la
Kiinjili la Kiluteri Tanzania (KKK) Dayosisi ya
Mashariki na Pwani, (DMP) anatafuta watoto
waliotoroshwa kwa maelekezo ya Malasusa na
Jeshi la Polisi, anandika Josephat Isango.
Akizungumza na MwanaHALISI online baada ya
kuachiwa huru kutoka polisi kwa tuhuma za
kushambulia, amesema watoto wake
walichukuliwa na raia mmoja mjerumani
aliyeolewa na mtanzania, anaitwa Caroline
Shedafa.
Caroline Shedafa ametuhumiwa kuwa ametumia
mwanya wa malalamiko ya Mwakilima na
Malasusa kwa sababu ya urafiki alifanikiwa
kuwatorosha watoto hao na kwamba ana mpango
wa kuwasafirisha kwenda nje ya nchi wakati
wowote.
MwanaHALISI limemtafuta Shedafa kwa tuhuma
hizo, alipokea simu na baada ya kuambiwa kuwa
anaongea na MwanaHALISI alikata simu na
kukataa kuongea suala hili na mwandishi.
Malasusa anadaiwa kuwa anadaiwa kushirikiana
na mfanyakazi wa hospitali ya Muhimbili
anayeitwa Julieti, aliyewaambia ndugu wa mume
anayenyang’anywa mke wake na malasusa kuwa
atakiona.
“Huyu kaka anajidai mjuaji, hapti kitu, utaratibu
uko tayari wa kuwasafirisha watoto kwenda nje
ya nchi na hatawaona tena, ataishia kuwasikia tu,
mimi ni mtu wa Karibu na Askofu Malasusa ndo
nawaambia”. Alinukuliwa dada huyo akiongea
kwa ujasiri.
Hadi sasa watoto wanaotafutwa na baba yao
ambao Jeshi la Polisi linadaiwa kushirikiana na
Malasusa licha ya taarifa zao kufika polisi kituo
cha Wazo na kutochukuliwa hatua ni Sijenuni,
Sephania, na Simon wote wanadaiwa kuwa
watoto wa Venance Mwakilima.
Taarifa za leo usiku zilizofikiwa MwanaHALISI
online zinadai kuwa baadhi ya Maaskofu Jijini
Dar es Salaam wameamua kujitokea kulinda
heshima ya uaskofu baada ya kudhalilishwa na
Malasusa.
Maaskofu ambao hawakupenda kutajwa majina
yao kwa kuwa si wasemaji wa vikao halali
wamesema “hili suala tunalichukua,
Malasusa ana tuhuma nzito nchini, na baada ya
gazeti kuandika watu wamejitolea kujieleza
tunaomba muda kesho (Jumanne) tutaliongelea
hadharani baada ya kukutana na mume wa me.
Aidha Malasusa hakupatikana kwenye simu zake
wala kujibu ujumbe wa simu aliotumiwa tangu
juzi wakati gazeti la MwanaHALISI likiendelea
kufuatilia sakata hili.
Taarifa ambazo mwandishi anazo zinadai
viongozi wakubwa wa serikali wanaingilia suala
hili, zinafuatiliwa na zitaandikwa kwenye gazeti la
MSETO.chanzo godlack peter mtenga.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top