Kagera yapiga stopu sukar kuuzwa jumla jumla sasa kuuza reja reja.
Serikali mkoani Kagera imesitisha uuzwaji
wa sukari kwa biashara ya jumla, badala
yake imetenga maduka maalumu kwa kila
kata yatakayohusika kuwauzia wananchi
sukari kwa bei elekezi ya Serikali,lengo
likiwa ni kuondoa uhaba wa sukari na
kuwaondolea kero wananchi.
Kwa mujibu wa Afisa Biashara mkoani
hapa Isaya Tendega,uamuzi huo
umefikiwa mara baada ya kubaini kuwa
wapo baadhi ya wafanyabiashara wa
maduka ya jumla wanaotumia changamoto
ya upungufu wa sukari na kuiuza kwa bei
ya juu tofauti na bei iliyoelekezwa na
Serikali.
Tendega amesema kuwa hali ya Sukari
iliyoko katika kiwanda cha kuzalisha
Sukari cha Kagera ni yakutoshereza kwa
wananchi wa mkoa wa Kagera,ingawa
changamoto ya kuwepo uhaba wa Sukari
inachangiwa kwa kiwango kikubwa kwa
Wafanyabiashara kutoka nje ya mkoa
kufika Bukoba kuchukua Sukari kwa bei
yeyote wanayoitaka wao na kuufanya
mkoa kukabiliwa na changamoto hiyo.
Amesema maduka maalumu husika
yatakuwa yakisimamiwa na halmashauri
za wilaya na Manispaa,hivyo kuwaomba
wananchi wa mkoa wa Kagera,kuwa na
uvumilivu kwa hatua ya utekelezaji huo
inaendelea na kufikia Mei 2(Jumatatu)
huduma ya maduka hayo itakuwa imeanza
kuwahudumia wananchi.
Uhaba wa Sukari mkoani Kagera imekuwa
changamoto kwa wananchi,hali
inayosababisha wauzaji wa jumla kuuza
sukari kwa bei ya 125,000/ huku bei ya
rejareja ikiuzwa kati ya shilingi 2,400 hadi
2600/=huku lawama nyingi zikielekezwa
kwa Serikali.
M
0 comments :
Post a Comment