Breaking News
Loading...

Advert

Friday, April 29, 2016

Wamachinga wa ubungo kuhamia soko la mawasiliano.soma zaidi.

Meya wa Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar
es Salaam Mstahiki Boniface Jacob
amezua taharuki kwa wamachinga wa
ubungo na kukimbia biashara zao
wakiambatana naye mithili ya
Maandamano mara baada ya kutangaza
kufuta umiliki wa vizimba na mabanda
takriban 100 yaliyokuwa yakimilikiwa na
watendaji na Madiwani wa Manispaa ya
Kinondoni katika soko la Mawasiliano
Maarufu kama Simu 2000 akiagiza
wapewe bure.
Mstahiki Jacob aliyefuatana na watendaji
wa Manispaa hiyo alitembea kwa miguu
akiongea na wamachinga mmoja mmoja
na makundi kuanzia Ubungo Plaza hadi
ubungo maji akiwaelimisha umuhimu wa
oparesheni ya kuwaonda barabarani ikiwa
ni sehemu ya maandalizi ya ujenzi wa njia
za juu na kuanza kwa usafiri wa mabasi
ya kasi Dart ambao hali ilibadilika pale
alipotaja Manispaa kuwa na masoko 26
yaliyohodhiwa na viongozi kwa kuingia
Mikataba ya kupangisha wakati
wamejiagawia bure.
Aidha Mstahiki Meya Boniface Jacob
amesema katika kuhakikisha wafanya
biashara wadogo wanatengewa maneo
yao watafanya uhakiki katika masoko yote
kubaini viongozi na watendaji
waliojimilikisha na kuwanyang’anya ili
masoko yatumiwe na walengwa ikiwa ni
hatua ya kuboresha mazingira ya jiji huku
mtendaji wa kata ya ubungo Bw. Gilbati
Mushi akieleza hatua hiyo kudhirisha
utawala bora.
Chanzo: ITV

0 comments :

Post a Comment

Back To Top