Breaking News
Loading...

Advert

Friday, April 29, 2016

Harry kitily na wenzeka wawil warudishwa rumande hadi tena mei3.

Aliyekuwa Kamishna wa TRA, Harry Kitilya,
Sioi Solomoni na aliyekuwa afisa
mwandamizi wa benki ya Stanbic tawi la
Tanzania pia ni mshindi wa taji la Miss
Tanzania 1996, Shose Sinare April 27
2016 walikosa dhamana kutokana na
upande wa Jamhuri kukata rufaa
mahakama kuu kupinga maamuzi ya
kupewa dhamana.
Leo April 29 2016 kesi hiyo ilitajwa
kusikilizwa Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu jijini Dar es salaam ambapo awali
Hakimu Mchauru alitoa maamuzi ya
kuahirishwa kwa kesi hiyo mpaka Mei 12
mwaka huu, sababu ni kutokana na jalada
halisi la kesi kupelekwa mahakama kuu
baada ya kukatwa kwa rufaa ya kufutiwa
shitaka namba nane la utakatishaji fedha.
Muda mfupi baadae majira ya saa 4;30
asubuhi walirudishwa tena mbele ya
Hakimu Mchauru baada ya kupata amri
kutoka kwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu
Kanda ya Dar es salaam akitamka kesi
hiyo itajwe Mei 3 mwaka huu badala ya
mei 12, aliyoipanga awali.
Hakimu Mchauru amesema sababu za
kupewa amri hiyo hazijui, hivyo kesi
itatajwa tena Mei 3 mwaka huu na yale
yaliyozungumzwa asubuhi yatabaki kama
ilivyo, watuhumiwa wote wamerudishwa
rumande.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top