Chadema yajitoa kwenye mchakato wa katiba mpya.soma zaid.
amesema kuwa Katiba Mpya inayotokana na
maoni ya wananchi ndiyo msingi imara pekee
unaoweza kuweka mifumo na taasisi kwa ajili
ya maendeleo ya kweli yatakayogusa maslahi
ya Watanzania wote badala ya nchi
kuongozwa na kauli za viongozi, Kutokana na
umuhimu huo wa kuzingatia maoni ya
wananchi yanayobeba matakwa yao katika
mchakato wa Katiba Mpya, amesema kuwa
Chadema hakitashiriki kura ya maoni ya
Katiba Mpya Inayopendekezwa ambayo
ilipitishwa na Bunge Maalum la Katiba baada
ya kubadili na kuondoa mapendekezo
yaliyotolewa na wananchi kwenye Rasimu ya
Pili ya Katiba Mpya.
Badala yake, Chadema kitaendelea kuweka
agenda ya kupigania Katiba Mpya na bora
katika vipaumbele vyake, kwa sababu itatibu
vidonda na kumaliza makovu yaliyoko katika
jamii kutokana na matatizo mbalimbali kama
vile ukosefu wa haki, migogoro ya ardhi,
wananchi kukosa huduma za msingi za kijamii
zikiwemo elimu, maji na afya.
Dkt. Mashinji ameyasema hayo leo jijini Dar es
Salaam alipoukaribisha ujumbe wa Chama cha
Centre Party cha Norway uliofika ofisini kwake
jijini Dar es Salaam kutia saini makubaliano ya
ushirikiano kati ya vyama hivyo kwenye Mradi
wa Elimu ya Demokrasia awamu ya pili
unaofanyika Wilaya ya Mtwara Vijijini.
Dkt. Mashinji pia amekishukuru chama hicho
kwa kusaidia kutoa elimu ya uraia kwa
Watanzania hususani maeneo ya vijijini katika
mradi ambao unahusisha vyama vyote vya
siasa vyenye uwakilishi ndani ya Bunge, huku
akisisitiza kuwa Chadema kiko tayari kwa
ushirikiano unaozingatia maslahi na matakwa
ya wananchi hasa katika kukuza uelewa wa
kudai haki, demokrasia na uongozi bora ndani
ya nchi.
“Suala la Katiba Mpya inayotokana na maoni
ya wananchi kama ilivyowasilishwa kwenye
rasimu ya pili na Tume ya Mabadiliko ya
Katiba Mpya ni agenda muhimu kwa
Watanzania wapenda nchi yao na sisi ni
kipaumbele kwa mwaka huu na kuendelea hadi
hapo nchi yetu itakapopata Katiba Mpya ya
Wananchi.
Amesema “Jana na leo tumewasikia baadhi ya
viongozi wa serikali wakisema kuwa
wanajiandaa kuitisha kura ya maoni…
hatutashiriki kura ya maoni ya Katiba Mpya
Inayopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba.
Tunajua Watanzania wengi wanataka Katiba
Mpya iliyotokana na maoni yao, si ile
iliyochakachuliwa bungeni.
Aliongeza kuwa “Katiba Mpya iliweka masuala
kuhusu haki za wananchi, kuimarisha misingi
na kuweka mifumo ya demokrasia na uongozi
bora, walau kwa kuanzia. Hatuwezi kusema
sasa tutatumia mikakati gani kuwahamasisha
Watanzania kuidai Katiba Mpya…tutajua
namna ya kuvuka tukishafika mtoni,”
Aidha, Katibu Mkuu Dkt. Mashinji amesisitiza
kuwa suala la nchi kuwa na misingi na mifumo
imara ya demokrasia na uongozi bora ni
muhimu kwa Tanzania, katika wakati ambapo
nchi inaelekea kwenye uchumi mkubwa wa
nishati ya gesi na mafuta, akisema vinginevyo
ni hatari iwapo taifa lenye utajiri mkubwa wa
rasilimali, litaendelea kuwa na wananchi
waliokata tamaa kutokana na mfumo mbovu
uliopo.
Kwa upande wake ujumbe huo uliokuwa
ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Centre Party,
Knut Olsen, umesema kuwa chama hicho
kinashukuru kwa mradi huo kuingia katika
hatua ya pili kuanzia mwaka 2016-2019 huku
hatua ya kwanza ikiwa na mafanikio makubwa
katika jamii ya wananchi wa maeneo ya
pembezoni.
“Kama unavyojua, mradi huu kupitia TCD
unahusisha vyama vyote vyenye uwakilishi
ndani ya bunge, na lengo letu ni kuwajengea
uwezo viongozi wa vyama hasa wanawake na
vijana katika ngazi ya jamii kwenye vitongoji,
vijiji, kata na bunge ili waweze kushiriki
mchakato wa maamuzi. Tunatarajia kuendelea
kupata ushirikiano katika hatua ya pili,”
amesema Inger Bigum, ambaye ni Meneja wa
Mradi hapa nchini.
Wengine waliokuwa katika ujumbe huo wa
Centre Party ni pamoja na Vijana Sara Hamre
Katibu Mkuu wa, Katibu Mkuu wa Wanawake,
Eline Stokstad-Oslan na Kristin Madsen Katibu
Mkuu wa Wazee, Mradi huo wa Elimu ya
Demokrasia katika Wilaya ya Mtwara Vijijini
unaohusisha vyama vyenye uwakilishi bungeni
kupitia Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD)
chini ya ufadhili wa chama hicho, katika
awamu ya kwanza ulihusisha kata za
Msangamkuu, Nanyamba, Ziwani na
Mbembaleo na katika sasa awamu ya pili
utakuwa katika kata za Mkunwa, Tangazo,
Mayanga na Madimbwa.
0 comments :
Post a Comment