Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, April 21, 2016

Mabasi ya daladala Dar marufuku route katikati ya jiji kabla ya mei10.


Hayo yamesemwa leo na Msemaji wa
Mradi wa Mabasi yaendayo Kasi(DART)
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa
Mabasi Mkoa wa Dar-es-salaam
(Darcoboa), Sabri Mabrouk. Mabrouk
amesema wamiliki wa daladala
zinazofanya safari zake katika ya Jiji
walishalipwa fidia ya kubadili route.
"Wamiliki wote wa mabasi wameshalipwa
fedha zao tangu December mwaka jana,
hakuna anaedai na tumewapa siku saba
kuondoka barabarani kabla ya Mei
10,"alisema Mabrouk.
Jiandaeni kusikia wengine wanalalamika
hawajalipwa na wataamua kupinga agizo
hili hata kwa kwenda mahakani.
MPANGILIO WA RATIBA ZA MABASI YA
MWENDO KASI KESHO.
MABASI YATAANZA SAFARI SAA KUMI NA
MBILI KASORO ROBO KUTOKEA DEPOT YA
JANGWANI KWA MPANGILIO UFUATAO.
1. RUTI YA KIMARA- KIVUKONI Mabasi
Sita (6). Kati ya mabasi Hayo sita wakati
wa Kutoka Jangwani matatu yataenda
Kimara na Matatu Kivukoni.
2. RUTI YA KIMARA - KARIAKOO Mabasi
Sita (6). Kati ya hayo Matatu yataelekea
Kariakoo na Matatu Kimara.
3. RUTI YA UBUNGO - KIVUKONI Mabasi
nane (8). Kati ya hayo Mabasi Manne
yataelekea Ubungo na Manne Kivukoni.
4. RUTI YA UBUNGO - KARIAKOO Mabasi
nane (8). Kati ya hayo Mabasi manne
Yataenda Ubungo na Manne yataenda
Kariakoo.
5. RUTI YA UBUNGO - MOROCCO Mabasi
nane (8). Kati ya hayo Manne yataenda
Ubungo Manne yataenda Morocco.
6. RUTI YA MOROCCO - KARIAKOO
Mabasi sita (6). Kati ya hayo mabasi
Matatu Morocco na Matatu Kariakoo.
7. RUTI YA MOROCCO - KIVUKONI Mabasi
nane (8). Kati ya Hayo Mabasi Manne
yataenda Moroco na mabasi manne
Kivukoni.
DESPATCH PLAN SAA KUMI NA MBILI
KAMILI.
1. Kimara Terminal Mabasi Sita (6)
2. Ubungo Terminal Mabasi kumi na mbili
(12)
3. Morocco Termial Mabasi kumi na moja
(11)
4. Kariakoo Terminal Mabasi kumi (10)
5. Kivukoni Terminal Mabasi kumi na
moja (11)
JUMLA.NI MABASI HAMSINI (50) chanzo jamii forums.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top