Watumishi hewa waongezeka Arusha kutoka 270 na kufikia 350.soma zaid.
adi ya watumishi hewa katika mkoa wa Arusha
imeongezeka kutoka 270 na kufikia 350.
Akikabidhi taarifa ya matokeo ya uchunguzi wa
Tume iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha
Daud Felexs Ntebenda,Katibu Tawala Msaidizi
anashughulikia utawala na rasilimaliwatu mkoa
wa Arusha Bw Richard Kwitega amesema
asilimia kubwa ya watumishi hewa
walioongezeka wanatoka wilaya za Karatu na
Arumeru.
Akizungumza baada ya kupokea ripoti hiyo
inayoonyesha mishahara hiyo hewa ililipwa
kuanzia mwezi July 2014 hadi sasa,Mkuu wa
Mkoa wa Arusha Daudi Ntebenda ametoa siku 14
kwa wakurugenzi kuhakikisha fedha ziliotolewa
zinarudishwa.
Pia amewataka wakuu wa wilaya kuhakikisha
ndani ya siku hizo wanampatia taarifa ya hatua
za kisheria zilizochukuliwa kwa watumishi
waliohusika.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bw Adolfu
Mapunda amesema hadi sasa inaonyesha kuwa
zaidi ya bilion 1.5 zimelipwa kwa watumishi hewa
katika Mkoa wa Arusha.
Like
0
0 comments :
Post a Comment