Maghala la IS yasambaratishwa na vikosi vya kijesh vya marekani.
Hadi dola milioni 800 fedha taslimu
zinazodhibitiwa na kundi la wapiganaji la Islamic
State zimeharibiwa katika mashambulizi ya
angani, afisa mmoja wa jeshi la Marekani
amesema.
Meja Jenerali Peter Gersten ambaye amepiga
kambi nchini Baghdad amesema kuwa Marekani
imeripoti kuyalenga maghala yanayoweka fedha
hizo.
Pigo hilo kwa IS limesababisha kutoroka kwa
wapiganaji wake huku idadi ya wale wanaojiunga
na kundi hilo pia ikipungua.
Mwaka 2014 ,idara ya fedha nchini Marekani
ilisema kuwa kundi la Islamic State ndilo
linalofadhiliwa sana duniani.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari Gersten
ambaye ni naibu kamanda wa operesheni na
intelijensia katika kikosi cha Marekani,amesema
kuwa takriban makombora 20 ya angani
yaliolenga maghala ya fedha ya kundi hilo
yamerushwa.
Hatahivyo hakuelezea vile Marekani ilivyogundua
ni pesa ngapi zilizoharibiwa.
Katika kisa kimoja amesema kuwa takriban dola
milioni 150 ziliharibiwa katika nyumba moja mjini
Mosul nchini Iraq.
0 comments :
Post a Comment