Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, April 27, 2016

Jiji la Dar es salaam kuchunguza mali zake .soma zaid.

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam,
Isaya Mwita akizungumza na waandishi
wa habari jijini Dar es Salaam leo
BARAZA la Madiwani la Jiji la Dar es
Salaam limeunda kamati ya kuchunguza
mali za jiji hilo kutokana na mali hizo
kugubikwa na mbinu chafu na jiji
kushindwa kunufaika mali hizo.
Akizungumza leo na waandishi habari
jijini Dar es Salaam, Mstahiki Meya wa Jiji
la Dar es Salaam, Isaya Mwita amesema
kuwa kamati hiyo lazima ichambue mali
hizo na kama ziko kwenye mikataba nazo
ziangaliwe jinsi walivyoingia.
Amesema kuwa katika mali hizo ni
pamoja na vibanda 130 vilivyo katika
Benjamin Mkapa Kariakoo waliopanga
vibanda hivyo wanalipa sh.30,000
ambapo kwa kiwango hicho ni kidogo
sana kutokana eneo vilipo.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top