Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, April 27, 2016

Ukawa Dar es salaam waikalia kooni kampuni ya UDA-TR.soma zaid.



HALMASHAURI ya Jiji la Dar es Salaam
imewakaanga wanaotajwa kumiliki Shirika la
Usafiri Dar es Salaam (UDA) bila kufuata
utaratibu,
Hatua hiyo imekuja baada ya Halmashauri ya
Jiji la Dar es Salaam inayoongozwa Ukawa
kuzuia Sh. 5 bilioni, fedha mali ya Kampuni
ya Simon Group Limited.
Mama Salma Kikwete, Mke wa Rais Mstaafu,
Jakaya Kikwete na Ridhwan Kikwete, mtoto wa
rais huyo na Prof. Juma Kapuya, aliyekuwa
Mbunge wa Urambo Magharibi wanatajwa kuwa
miongoni mwa wana hisa kwenye shirika hilo.
Simon Group Limited ililipa fedha hizo kwa
halmashauri hiyo ikiwa ni sehemu ya malipo ya
ununuzi wa hisa za UDA.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam leo, Saed Kubenea, Mbunge wa Jimbo la
Ubungo amesema halmashauri haikuuza UDA
licha ya Simon Group Limited kudai kununua.
“Kwanza tunataka mtambue halmashauri
haikuuza UDA kwa kuwa, Simon Group Limited
wametumia hati ya UDA – mali ya wananchi
kufanya biashara. Haturudishi fedha hizi mpaka
tufanye hesabu, tujue kampuni hii imepata faida
kiasi gani.
“Hata katika mradi wenyewe wa UDA-TR,
kumesheheni utapeli. Unaoitwa mkutano mkuu
maalum wa wana-hisa wa tarehe 10 Juni 2011,
uliosimamiwa na Didas Masaburi, aliyekuwa Meya
wa Jiji kuidhinisha pamoja na mengine, uuzaji wa
hisa za UDA, haukuwa halali,” amesema
Kubenea.
Kubenea amesema, mkutano uliokabidha UDA
kwa Simon Group uliitishwa bila baraka za wenye
mali – Baraza la Madiwani la Jiji na Msajili wa
Hazina na kwamba, ulihudhuriwa na watu wanne
tu
“Watu hawa ni Dk. Didas Masaburi mwenyewe
ambaye alikuwa mwenyekiti; Mkurugenzi wa
Simon Group, Robert Kisena ambaye alikuwa
katibu; Mwanasheria wa jiji, Isaac Nassor
Tasinga na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, Phillip
Mwakyusa,” amesema Kubenea.
Amesema, kwenye mkutano huo Masaburi
alitangaza Kampuni ya Simon kuwa ‘imetimiza
masharti yote ya mkataba wa kupewa hisa, mali
na uendeshaji wa UDA.’
Ameeleza kuwa, mwaka 1983, Msajili wa Hazina
alitoa asilimia 51 ya hisa na kuipa Halmashauri
ya Jiji huku Serikali Kuu ikibakiwa na asilimia 49
na kwamba, shirika hili liliwekwa katika orodha ya
mashirika ya kurekebishwa na serikali mwaka
1997.
“Taarifa ya serikali ya tarehe 3 Agosti 2011
kwenda Kamati ya Bunge ya Miundombinu
inaeleza mkutano huo ulikuwa batili kwa kuwa,
ulikiuka Katiba ya UDA, kifungu namba 45
kutokana na kutotimia kwa akidi na kukosekana
kwa msajili wa hazina,” amesema Kubenea.
Taarifa hiyo imeeleza, kikao hicho hakikuwa na
mamlaka ya kufanya uamuzi, na kuwa maazimio
yote yaliyofikiwa yalikuwa batili.
“Kwa taarifa hii pekee, serikali ilipaswa kuiondoa
Simon Group kwenye uendeshaji wa UDA
ikiwemo kukodishwa mali zake, hadi hapo
uchunguzi wa suala hilo utakapokamilika.
Haikufanya hivyo,” amesema Kubenea.
Kubenea amesema, kwa taarifa hiyo pekee
ilitosha serikali kuchunguza na kuwachukulia
hatua wote waliohusika, hasa kwa kuzingatia
kuwa, kabla ya kikao hicho, tayari Masaburi
alishapokea barua ya tarehe 28 Februari 2011
kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu iliyomuagiza
kusitisha mara moja mchakato wa kuuza hisa za
serikali ambazo hazijagawiwa.
Akinukuu barua kutoka kwa Waziri Mkuu yenye
Kumbukumbo Na. 185/295/01/27, amesema
Masaburi na wenzake waliendesha mkutano huo
wakiwa na kabrasha la Katiba ya UDA ambayo
vipengele vyake vilikuwa vinakataza
walichokifanya.
“Kipengele cha 2.0 cha mkataba kinaeleza
mauzo ya hisa 7,880,303 ambazo
hazijagawanywa ambapo kwa majibu wa
kipengele cha 2.2, mnunuzi alipaswa kulipa kwa
awamu kiasi cha Sh. 1.1 bilioni,” amesema.
Aidha, anasema malipo ya kwanza ya Sh. 285. 6
milioni sawa na asilimia 25 ya malipo yalipaswa
kufanywa katika kipindi cha siku zisizozidi 14
tangu mkataba kufungwa.
Lakini Simon Group haikulipa kiasi kamili kwa
mujibu wa mkataba na hata kiasi ilichotoa ilikilipa
nje ya siku zilizotajwa na mkataba.chanzo mwanahalisonline.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top