Majambazi wavamia maduka na kuua mtu mmoja kagera.soma zaid.
Majambazi waliosadikiwa kuwa na Silaha za
kivita,wanatafutwa na Jeshi la Polisi mkoani
Kagera,kutokana na kuvamia maduka katika kijiji
cha Nyakaiga wilayani Karagwe na kusababisha
kifo cha mtu mmoja baada ya kupigwa risasi
mgongoni.
Tukio hilo,lilitokea majira ya saa 2:30 jana (April
26)ambapo kundi hilo la majambazi lilivamia
katika kijiji hicho na kuanza kufyatua risasi za
hapa na pale hali iliyosababisha risasi moja
kumpata mkazi mmoja kijiji hicho Ndyamukama
Theonest(40)iliyompata sehemu ya mgongoni na
kusababisha kifo chake papo hapo.
Kwa mujibu wa Kamanda wa jeshi la Polisi
Mkoani hapa Augustine Ollomi,pamoja na
majambazi hao kusababisha kifo na kuleta
taharuki kwa wananchi katika kijiji hicho pia,
wakifanikiwa kupora fedha kutoka kwenye
maduka hayo ambazo hazijajulikana ni kiasi gani.
Ollomi alisema mara baada ya tukio
hilo,majambazi hao walitokomea polini huku
uchunguzi wa Jeshi la Polisi ulibaini maganda 21
ya risasi yaliyotumika na risasi 2 ambazo zilikuwa
bado hazijakutumika hata hivyo uchunguzi wa
kinterejensia unadhihihirisha kuwa kundi la
majambazi hao,halikuwa la wenyeji wa eneo
husika.chanzo radio one
0 comments :
Post a Comment