Marco jidendela mkazi wa simiyu atupwa jela maisha kwa kulawiti mtoto wa miaka 9.
Mkazi wa kijiji cha Nyabubinza wilayani Maswa
mkoani Simiyu, Marco Jidendela (25) ametupwa
jela maisha baada ya kupatikana na hatia ya
kulawiti mtoto wa miaka 9.
Hukumu hiyo imetolewa jana na Hakimu Mkazi
wa Mahakama ya wilaya ya Maswa,Tumaini
Marwa baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa
na upande wa mashitaka.Awali ilidaiwa
mahakamani hapo na Mwendesha mashitaka,
Mkaguzi wa Polisi,Nassib Swedy kuwa
mshitakiwa alitenda kosa hilo Januari 8 mwaka
huu majira ya saa 4:30 asubuhi katika kijiji cha
Nyabubinza.Mwendesha mashitaka huyo alidai
kuwa siku ya tukio mshitakiwa alimshika kwa
nguvu mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 9
(jina linahifadhiwa) ambaye alimkuta akichunga
ng’ombe na kumweleza ya kuwa achague moja
amuue au amlawiti.
Kufuatia hali hiyo alitimiza adhima yake kwa
kumwingilia kinyume cha maumbile na
kumsababishia mtoto huyo michubuko na uvimbe
katika sehemu yake ya njia ya haja kubwa
kinyume na kifungu cha 154(1)(a) cha kanuni ya
adhabu sura ya 16.
Nassib aliiomba Mahakama itoe adhabu kali kwa
mshtakiwa ili liwe fundisho kwa watu wengine
wenye tabia kama hizo.
0 comments :
Post a Comment