miezi 15 kuanzia sasa mishahara ya watumishi wa umma kuwa na uwiyano sawa.
IKU chache baada ya Rais Dk. John Magufuli
kutoa agizo la kupunguza mishahara mikubwa ya
watendaji wa mashirika ya umma, hatimaye
Serikali kupitia Bodi ya Mishahara imeanza kazi
ya kufanya marekebisho hayo.
Hatua hiyo imekuja baada ya Rais Magufuli,
kuagiza kushushwa kwa viwango vya mishahara
ya viongozi wa mashirika ya umma ambapo
wengine hulipwa Sh milioni 36 hadi milioni 40
kwa mwezi.
Akizungumza jana jijini Dar es
Salaam, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Angellah Kairuki, alisema katika kipindi cha
miezi 15 kuanzia sasa mishahara ya watumishi
hao itapunguzwa na kuwa yenye uwiyano.
“Katika kuhakikisha agizo hilo linatekelezwa
tunayo Bodi ya Mishahara ambayo ilianzishwa
katika Serikali ya awamu ya nne na jukumu lake
kubwa ni kufanya mapitio ya mishahara
mbalimbali na kuhakikisha mishahara ya
watumishi wa umma haipishani sana.
“Hatua ambazo tumeanza kuzitekeleza, tayari
mamlaka zetu zimeanza kukutana kupitia
Utumishi, Hazina na Msajili wa Hazina ili
kuangalia namna ya kulitekeleza agizo hilo,”
alisema Waziri Kairuki.
Alisema kutokana na hali hiyo mamlaka hizo hivi
sasa zinaangalia mishahara ya taasisi mbalimbali
na watumishi ili kuweza kubaini wale wanaolipwa
zaidi ya Sh milioni 15 ni wangapi na itakatwa
vipi.
Akizungumzia taasisi zinazozalisha kwa kiwango
kikubwa na kuwa na uwezo wa kujiendesha,
Waziri Kairuki, alisema Bodi ya Mishahara hivi
sasa ina jukumu la kuangalia uwiano baina ya
mtumishi wa umma na mashirika ya Serikali.
“Unakuta mtumishi wa taasisi X kiwango chake
cha elimu, uzoefu, ujuzi, muda wa kuingia kazini
pamoja na kazi anayoifanya ni sawa na ya
mtumishi wa taasisi Y lakini unakuta mtumishi X
analipwa mshahara mkubwa zaidi ya mara tano
ya mtumishi jambo ambalo si haki katika
utumishi,” alisema.
0 comments :
Post a Comment