Breaking News
Loading...

Advert

Tuesday, April 5, 2016

Rais wa Zanzibar Dk.shein Afuata Nyao za Rais Maguful.soma zaid.

Rais Shein apiga marufuku safari nje ya
Z’bar zisizo za lazima na kuondoa posho
wakati wa muda wa kawaida wa kazi
kupunguza matumizi ya serikali. Azindua
rasmi Baraza la Wawakilishi.
===================
Mheshimiwa Spika,
Vile vile, katika jitihada zetu za kusimamia
matumizi bora ya fedha za umma, Serikali
itadhibiti na kuzuwia safari za nje za
kikazi zisizo za lazima. Semina,
kongamano na mikutano inayofanywa kwa
kutoa posho wakati wa saa za kazi,
itawekewa utaratibu mpya. Serikali
itahakikisha kuwa ubora wa miradi
inayotekelezwa na ununuzi wa vifaa na
huduma mbali mbali zinalingana na
thamani ya fedha zilizotumika (Value for
Money).
Zipo taarifa kwamba kuna ubabaishaji
mkubwa unafanyika, katika ununuzi wa
vifaa na nyenzo. Ni jukumu la Watendaji
Wakuu na wale wote wenye dhamana ya
manunuzi na kuidhinisha miradi,
kuzingatia Sheria Namba 9 ya 2005 ya
Manunuzi na Uondoshaji wa Mali za
Umma, wahakikishe kwamba taratibu zote
za manunuzi zinafuatwa.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top