Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, April 20, 2016

Mkurugenzi Dar aliyesimamishwa kazi na Rais amefunguka na haya.soma zaid.

Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam,
Wilson Kabwe amesema uchunguzi wa
tuhuma zilizomfanya Rais John Magufuli
kumsimamisha kazi jana utabainisha
ukweli huku akihoji; “ikiwa itabainika
kwamba nilionewa nitalipwa fidia?”
Alisema hayo mara baada ya Dk Magufuli
kutangaza kumsimamisha kazi wakati wa
uzinduzi wa Daraja la NSSF Kigamboni
ambalo sasa litaitwa Daraja la Nyerere
baada ya kumwita Mkuu wa Mkoa wa Dar
es Salaam, Paul Makonda kueleza tuhuma
dhidi ya mkurugenzi.
Alipoulizwa jana, Kabwe alisema hakuwa
na taarifa za kusimamishwa kwake na
mazungumzo yake na mwandishi wetu
yalikuwa kama ifuatavyo:
Mwandishi: Habari mkurugenzi?
Kabwe: Salama.
Mwandishi: Tumepata taarifa za
kusimamishwa kwako kazi na Rais
kutokana na tuhuma zilizotolewa juzi na
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Makonda tunaomba maoni yako.
Kabwe: Sijasikia ndiyo kwanza unaniambia
wewe, kasema lini Rais?
Mwandishi: Leo wakati akizindua Daraja la
Kigamboni.
Kabwe: Alitamka palepale au?
Mwandishi: Ndiyo.
Kabwe: Sasa kama ameshasema yeye
ndiyo mkubwa mimi sina la kusema tena.
Mwandishi: Nataka kujua unazungumziaje
uamuzi huo?
Kabwe: Nimekwambia sina la kukwambia
kwa sasa lakini nimesema tu sina shida
na hilo, uchunguzi ufanyike nina uhakika
ukweli utajulikana tu. Lakini kama
ukijulikana na ikibainika nimeonewa je,
kuna fidia yoyote nitalipwa?
Chanzo: Mpekuzi.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top