Zitto afunguka haya kuhusu waziri kitwanga.soma zaid
Kumekuwa na maneno yanasemwa na mimi
kupuuza katika kipindi cha wiki kadhaa; kwamba
ninapanga kumhujumu Rais Magufuli katika kazi
zake. Maneno haya yanaenezwa na watu
wanaotumwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi Bwana Charles Kitwanga ( nina ushahidi
usio na mashaka wa Kitwanga kupanga vijana
wa wanaojiita wa UVCCM kufanya mikutano na
waandishi wa habari na anawalipa fedha kufanya
hivyo. Nataka ifahamike bila chenga kama
ifuatavyo:
1) Ninamwunga mkono Rais katika kazi ya
kusafisha Nchi. Hii ndio kazi nilikuwa nafanya
katika kipindi cha miaka 10 iliyopita. Nitakuwa
mtu wa ajabu sana nisipomwunga mkono Rais
katika vita dhidi ya Ufisadi. Hata hivyo, kamwe
sitasita kuweka wazi pale ninapoona Rais
anafanya makosa. Na nimekuwa nikisema wazi
wazi na kumkosoa Rais waziwazi. Lakini pia
nimekuwa nikimwambia Rais kwa njia nyengine
ambazo viongozi huwasiliana ninapoona
anafanya sivyo. Kukosoa ni kazi moja muhimu
sana na ya kizalendo kuliko lolote ambalo raia
anaweza kufanya kwa kiongozi wake. Kukosoa
Serikali ni uzalendo maradufu. Pale panapostahili
nitapongeza.
2) Namsihi Waziri Kitwanga amalize matatizo
yake yeye mwenyewe. Yeye kama mmiliki wa
Kampuni ya Infosys yenye mkataba na Serikali
katika Wizara anayoongoza sasa anapaswa aone
ni namna gani hana mgongano wa maslahi.
Waziri Kitwanga asitafute watu wa kuwatupia
lawama kwenye mambo yanayomhusu. Mimi
binafsi sijawahi kugombana na Charles Kitwanga.
Hajawahi kuwa rafiki yangu. Hajawahi kuni excite
kama Kiongozi ( kimsingi nashangaa mtu kama
yeye kuweza hata kuwa Waziri wa Wizara nyeti
kama hiyo) . Zaidi ya yote Waziri Kitwanga sio
'size yangu'. Kwa protokali za Uongozi, size
yangu mimi ni Rais Magufuli, bosi wake.
Naanzaje kuhangaika na Kitwanga? Ili iweje?
Namsihi asijipandishe chati kwamba mimi nataka
kumtoa. Ningetaka kumtoa wala asingejua maana
ningeshughulika na aliyemteua. Nasema haya
sababu amekaa na Waziri Mkuu na Wabunge
kadhaa akilalamika kuwa nataka kumtoa Uwaziri.
Asinipe dhambi, Uwaziri atatolewa na aliyemteua
kwa madhambi aliyofanya. Asitafute bangusilo!
3) Mimi kwa wiki kadhaa sasa nipo nje ya Nchi
( nchini Marekani katika Chuo Harvard kwa
masomo) . Sijui na sihusiki na njama zozote dhidi
ya yeyote. Kwanza hizo sio aina ya siasa
ninazofanya. Siasa ninazofanya ni Siasa za
Maendeleo ya Wananchi na sio Siasa za kuwinda
watu.
4) licha ya kuwa Kiongozi wa Chama, Mimi ni
Mbunge wa Chama Cha ACT Wazalendo. Kwa
hiyo nafuata maelekezo ya chama changu katika
kazi zangu. Chama changu katika Mpango
Mkakati wake kimeniagiza kufanya Siasa za
Maendeleo. Chama changu kinaunga mkono
juhudi zote za Rais kurejesha imani ya wananchi
kwa Serikali kwa kupambana na ufisadi. Hata
hivyo Chama Cha ACT Wazalendo kinamtaka
Rais ajenge mfumo imara wa kitaasisi ili
mapambano dhidi ya ufisadi yawe endelevu.
Hivyo, porojo za kwamba nataka kumwangusha
Rais ni porojo za watu wasionijua binafsi na
wasiojua misingi ya ACT Wazalendo
5) Nawasihi Watanzania wote a) kumdharau
Waziri Kitwanga na kumtaka ajibu tuhuma
zinazomkabili za Kampuni yake binafsi kufanya
kazi na Idara katika Wizara anayosimamia na
kwamba ajipime kama anatosha kuendelea
kumsaidia Rais kazi b) kuendelea kumwunga
mkono Rais katika vita dhidi ya ufisadi. Kama
nilivyosoma mwaka jana ' asiyemwunga mkono
Magufuli yupo upande wa mafisadi' c) kuepuka
siasa za porojo zinazoendeshwa na vijana
wanaotafuta nafasi za kuteuliwa na d) kutaka
umadhubuti wa kila jambo linasomewa ili
kuepuka kuonea watu.chanzo zitto fb.
0 comments :
Post a Comment