Ajari#gari laserereka wakati likiingia katika kivujo cha kigambon na kutumbukia ndani ya maji watu wawili wamefariki.soma zaid.
Watu wawili wamepoteza maisha baada ya
gari walilokuwemo kuserereka wakati
likiingia katika kivuko na kutumbukia
baharini eneo la Kivukoni, Dar es Salaam
leo. Gari hiyo aina ya Toyota Hiace ikiwa
na 2. Mwili wa dereva wapatikana, na
kikosi cha jeshi la zimamoto watafuta wa
pili.
Habari zaidi zinasema wavukaji hao
walikuwa ni waombolezaji na wametoka
Mkoani Morogoro kwenda msibani eneo
la KIGAMBONI na walikuwa hapo tokea
saa 9 za usiku na walikuwa wengi kwa
idadi ianyokadiriwa kuwa ni 15 na nia yao
ikiwa ni kusubiri PANTONI ya alfajiri
wawahi kuvuka nayo na walipokuwa hapo
(FERRY).
Walishuka katika gari waliyokuja nayo
kisha Watu wawili Dereva na Mwanamke
mmoja wakakodi gari nyingine aina ya
Toyota Hiace ili wakishavuka tu iwasaidie
kuwapeleka wote huko Msibani kisha wao
( Dereva na huyo Mwanamke ) wakaingia
katika hilo gari aina ya Toyota Hiace huku
wale Ndugu wengine wakikaa katika
PANTONI.
Safari ilipoanza tu hiyo Saa 10 alfajiri ya
kuvuka ndipo GHAFLA ile Hiace ikarudi
nyuma na KUZAMA majini wakati huo
PANTONI tayari imeshafika katikati ya
maji. Baada ya kuona hivyo yule Dereva
akafungua mlango haraka na kuruka
kutoka katika Gari na kuzama Baharini
huku mwanamke aliyekuwepo ndani ya
gari akashindwa kufanya lolote na
akazama na ile GARI.
Taarifa ziliwafikia WAOKOAJI wa
ZIMAMOTO Saa 11 alfajiri ndipo wao
wakawahi kufika eneo la tukio kuanza
uokoaji huku wakiomba tena MSAADA wa
Jeshi la Maji ( Navy ) ambapo walianza
kazi ya uokoaji tokea hiyo saa 11 na
ilipofika saa 3 asubuhi hii ndiyo
wakauona mwili wa yule Dereva ukielea
na wakautoa lakini mpaka sasa
WAOKOAJI hao wanaendelea kuusaka
mwili wa yule Mama
Lakini mpaka sasa hawajafanikiwa na
inasemekana kuwa huenda yule
mwanamke amezama na lile gari ( Hiace )
na sasa wanafanya utaratibu wa kulitafuta
hilo gari chini ya maji ili tu wautoe mwili
wa yule Mama ila kipingamizi kikubwa ni
hali ya mawimbi kwa sasa, mkondo wa
maji yale lakini kubwa zaidi kina kirefu
kilichopo pale ambapo ni takribani minazi
7 mpaka 9 ukiipanga kwa kuinyoosha.
0 comments :
Post a Comment