Breaking News
Loading...

Advert

Friday, April 29, 2016

Rais john maguful amelitaka jeshi la polisi kujirekebisha kwa kutekeleza wajibu wao.soma zaid

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelitaka
Jeshi la Polisi nchini na Ofisi ya Mwendesha
Mashitaka kujirekebisha kwa kutekeleza wajibu
wao huku wakitanguliza maslahi ya taifa.
Rais Magufuli ametoa maagizo hayo leo wakati
akifungua kikao cha kazi cha Makamanda wa
polisi wa mikoa, Mawakili wafawidhi wa serikali
wa Mikoa na Wakuu wa upelelezi wa Mikoa na
Vikosi, kinachofanyika kwa siku mbili Mjini
Dodoma.
Aidha, Rais Magufuli ameitaka Ofisi ya
Mwendesha Mashitaka kujipanga kufanya kazi
kwa ufanisi na ameelezea kusikitishwa na
vitendo vya serikali kushindwa katika kesi nyingi
mahakamani licha ya kuwa na wanasheria mahiri.
Hata hivyo Rais Magufuli amelipongeza Jeshi la
Polisi na ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka kwa
kazi kubwa wanayoifanya na ametaka apelekewe
mpango wa mahitaji yao ili atafute namna ya
kuimarisha vyombo hivyo.chanzo clouds.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top