Utumbuaji majibu unadhalilisha watumishi, nani kasema ?soma zaid.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu Mkuu
wa chama hicho Dk. Vicent Mashinji,
wakati alipokuwa akifungua kongamano
la Baraza la Vijana CHADEMA (Bavicha)
na Umoja wa wanachadema Vyuo vikuu
(Chaso) mjini hapa.
Dk. Mashinji alisema kuwa tangu aingie
madarakani Rais Magufuli amekuwa na
utaratibu ambao umepewa jina la
utumbuaji majipu ambao amekuwa
akiuendesha bila kufuata sheria za nchi.
Alisema kuwa pamoja na kuwa CHADEMA
wanaunga mkono kitendo cha
kuwashughulikia mafisadi pamoja na
watumishi wasio timiza majukumu yao
ipasavyo lakini hawakotayari kuendelea
kushuhudia ambavyo amekua akivunja
sheria za nchi.
“Watumishi wengi wamedhalilishwa na
serikali hii ambayo imekuwa ikitumia
mabavu kuwawajibisha watu bila kufuata
sheria za nchi,” alisema Dk, Mashinji.
“Suala la rushwa katika nchi ni jambo la
kimfumo ambapo kila unapoona kunamtu
katumbuliwa kwaajili ya rushwa basi kuna
idadi kubwa ya watu ambao wanashiriki
katika rushwa hiyo,” aliongeza Dk
Mashinji.
Aidha, alisema kuwa utaratibu wa Rais
kuwatumbua watumishi kwenye mikutano
ya hadhara kwa kutumia ushabiki wa
wananchi hauwezi kulisaidia taifa
kufanikiwa katika kuwaletea mabadiliko ya
kweli wananchi wake.
“Magufuli ametumbua watumishi wengi
sana tangu aingie madarakani lakini
niwaulize sukari imeshuka bei au mchele
umeshuka bei lakini kila siku tunasikia
watu wametumbuliwa bila kuwa na tija
kwa taifa,” alisema.
Aliwataka vijana wa vyuo vikuu nchini
kuungana na CHADEMA katika
kuhakikisha serikali inaruhusu
kuonyeshwa kwa vipindi vya Bunge moja
kwa mpja kama ilivyo kuwa hapo awali.
“Bunge maana yake ni mkutano wa
hadhara ambao wote tunatakiwa kushiriki
lakini kutokana na udogo wa eneo
wanakwenda wawakilishi wetu lakini na
sisi tunatakiwa tufuatilie kupitia runinga
zetu moja kwa moja ili tuweze kujua
kinachofanywa bungeni na wawakilishi
wetu,”alisema.
Pia aliwataka vijana kuacha ushabiki wa
kushabikia siasa bali waikosoe serikali ili
iweze kufanya kazi ambayo ni kuwaletea
maendeleo wananchi wake kwakua huo
ndio wajibu wake.
Akizungumza na wenyeviti wa CCM wa
Mikoa na Wilaya Ikulu, Rais Magufuli
alisema wanaotetea watu wanaotumbuliwa
na wao ni majipu hivyo ataanza
kuwachunguza.
Alisema inasikitisha kuona watu
wanatetea watumishi ambao wamekuwa
wakiwaibia watanzania miaka mingi lakini
wanapofukuzwa kazi wanalalamika.
“Kama wamekuwa wakiwaibia wananchi
hadharani nasisi tutawafukuza na
kuwatangaza hadharani, inasikitisha
kuona baadhi yetu tunatetea watu
wanaofukuzwa kazi,” alisema Rais
Magufuli
CHANZO: Nipashe
0 comments :
Post a Comment