Breaking News
Loading...

Advert

Monday, April 25, 2016

Wajue maasfisa waliofikishwa mahakani kwa kuomba rushwa.som zaid.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
TAKUKURU imewapandisha kizimbani maafisa
wawili, mmoja kutoka mamlaka ya mapato
Tanzania TRA Bw. Amani Simson Mkwizu na
mwingine wa Yono Action Mart Edward Magobela
wakituhumiwa kwa mashtaka matatu ya kuomba
rushwa ya fedha.
Washtakiwa hao wamefikishwa katika mahakama
ya hakimu mkazi kisutu mbele ya hakimu
Huruma Shahidi ambapo wakili wa Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa wakili Denis
Lekayo akisoma hati ya mashtaka mahakamani
hapo amedai kuwa washtakiwa hao walitenda
kosa hilo april 19 mwaka huu.
Katika shtaka la kwanza mahakama imeambiwa
kuwa washtakiwa hao walishawishi rushwa ya
shilingi milioni 50, shtaka la pili walishawishi
rushwa ya shilingi milioni 5 na shtaka la tatu
kupokea rushwa ya shilingi milioni 3 kutoka kwa
Mkurugenzi wa Kampuni ya Commercial, sells
and services Tanzania limited Bw. Glenk Clerk
ambapo wastakiwa hao walikuwa na lengo la
kupunguza gharama za ulipaji kodi kutoka kiasi
cha shilingi milioni 375 hadi milioni 100 toka
kampuni hiyo.
Hata hivyo washtakiwa wote hao kwa nyakati
tofauti walikana mashtaka hayo ambapo hadi ITV
inaondoka mahakamani hapo dhamana kwa
Washtakiwa hao zilikuwa wazi na walikuwa
wakihangaikia dhamana zao.kesi hiyo itatajwa
tena Mei 9 mwaka huu.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top