Breaking News
Loading...

Advert

Monday, April 25, 2016

Viongozi wa upinzani kenya wapigwa virungu na polisi baada ya kuandamana.soma zaid

Mshirikishe mwenzako
Viongozi wa mrengo wa upinzani nchini Kenya
(CORD) wamekabiliwa na maafisa wa usalama
baada yao kuandamana hadi makao makuu ya
Tume ya Uchaguzi (IEBC).
Maafisa wa usalama walianza kushika doria
mapema asubuhi jumba la Anniversary Towers,
lililo na afisi za IEBC.
Viongozi wa Cord wakiongozwa na waziri mkuu
wa zamani Raila Odinga na waziri wa zamani wa
mashauri ya kigeni Moses Wetangula walifika
mwendo wa saa tano wakiandamana na mamia
ya wafuasi lakini maafisa wa usalama
wakawazuia kuingia katika afisi hizo.
Mrengo huo unataka viongozi wa tume hiyo
waondolewa.
Wanasema viongozi hayo hawawezi kutegemewa
kuendesha uchaguzi mkuu huru na wa haki
mwaka 2017.
Viongozi wa CORD pia wamekuwa wakilalamikia
kukataliwa kwa baadhi ya saini zilizowasilishwa
na mrengo huo kuunga mkono ombi la
kuandaliwa kwa kura ya maamuzi ya
marekebisho ya katiba.
IEBC ilisema saini zilizokuwa halali hazikufika
saini milioni moja zinazohitajika kikatiba ndipo
ombi la marekebisho ya katiba kupitia kura ya
maamuzi likubalike.chanzo bbc swahil.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top