Zitto kabwe asema maneno haya kuhusu Rais. Soma zaid.
ZITTO Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha
ACT- Wazalendo amesema, Rais John Magufuli
anapapasa suala la ufisadi
Amesema, serikali yake bado haijachukua
hatua madhubuti katika vita dhidi ya rushwa
nchini licha ya ‘shangwe’ nyingi.
Ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati
akifungua mkutano wa Halmashauri Kuu ya ACT-
Wazalendo.
“Bado Rais hafanyi inavyopaswa, bado rais
anapapasa suala la ufisadi. Kuna mambo ya
muda mrefu ambayo tunaendelea kama nchi
kuyalipua lakini arais ameyakalia kimya. Mfano ni
suala la Tegeta Escrow,” amesema Zitto na
kuongeza;
“Bado mtambo wa IPTL upo chini ya matapeli na
kila mwezi serikali inawalipa matapeli hawa zaidi
ya Sh. 8 bilioni wazalishe au wasizalishe umeme.
“Hivi ndio vikundi maslahi katika sekta ya nishati
ambavyo bila kuvibomoa, rais ataonekana
anachagua katika vita hii.”
Zitto amesema, serikali imeficha inaowaita
madalali wa rushwa katika suala la hati fungani
ya Dola za Marekani 6 milioni.
Na kwamba, tayari kuna watu wamefikishwa
mahakamani lakini walioitoa rushwa hiyo ambao
ni Benki ya Standard ya Uingereza na waliopokea
ambao ni maofisa wa serikali, hawakupelekwa
mahakamani.
“Hati fungani hii ambayo serikali imeanza kulipa
riba yake ni ghali mno na imeongeza deni la taifa
kwa kiwango cha Sh. 1.2 trilioni bila ya riba.
Itakapofika mwaka 2020 ambapo tutakuwa
tumemaliza kulipa deni hili, tutakuwa tumelipa
zaidi ya Sh. 1.8 trilioni, shilingi bilioni 600 zaidi,”
amesema Zitto.
Zitto amesema, Watanzania zaidi ya 2000 duniani
kote wameweka saini kutaka Taasisi ya Rushwa
kubwa nchini Uingereza ( SFO ) kufungua upya
shauri hili na kuitaka Benki ya Standard iwajibike
kwa ufisadi huu dhidi ya nchi masikini ya
Tanzania.
Amesema Rais Magufuli angeongoza Watanzania
kukataa mikopo ya namna hiyo ambayo
inafukarisha nchi ingekuwa ni hatua kubwa lakini
Taasisi ya Kupambana na Rushwa (Takukuru)
wanaona sifa kuweka ndani watu kwa Sh. bilioni
12 bila kuwataja watu watakaofaidika na Sh.
bilioni 600 zaidi zitakazolipwa katika deni hilo.
“Ndio maama tunasema rais na serikali yake
bado hawafanyi ya kutosha katika vita dhidi ya
rushwa. Sio suala la kutumbua majipu tu, ni suala
la kuweka mfumo madhubuti ambao utazuia
rushwa kabisa.
“Chama chetu cha ACT -Wazalendo ni lazima
kiendelee kuunga mkono juhudi zozote za
kuondoa ufisadi nchini kwetu. Hata hivyo chama
chetu ni lazima kiendelee kukosoa serikali pale
ambapo tunapoona mambo hayaendi sawa.
“Tusiogope kuikosoa serikali kwa hoja kwani
kukosoa serikali ni tukio muhimu sana la
kizalendo,” amesema Zitto.
0 comments :
Post a Comment