Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, April 20, 2016

Watumishi Hewa 71 Dar ni Idad Ndogo sana mh.makonda aagiza Uhakiki Urudiwe Upya.soma zaid.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda amesema kuwa kazi ya kutafuta
watumishi hewa katika manispaa za jiji la
Dar es Salaam bado linaendelea baada
kubaini njia chafu wanazotumia watumishi
hewa hao.
Akizungumza leo na waandishi habari,
Makonda amesema kuwa Mkoa wa Dar es
Salaam ni kioo kwa nchi hivyo jitihada
zinaendelea ya kutafuta na kazi hiyo
itafanywa sekta kwa sekta.
Amesema kuwa Wakuu wa Wilaya katika
jiji la Dar es Salaam hakuna kufanya kazi
yeyote mpaka wamalize kutafuta
watumishi hewa kwa kutumia malipo ya
watumishi kutoka taasisi za fedha (Pay
Row).
Makonda amesema idadi ya watumishi
hewa 71 aliowasilisha kwa Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais –Tamisemi, Georgre
Simbachawene ni ndogo katika jiji la Dar
es Salaam hivyo kazi lazima iwe
endelevu.
Amesema kuwa watumishi Hewa
hawawezi wakawa wanalipwa mshahara
huku wanaofanya kazi kwa moyo mmoja
wanajisikia vibaya hivyo ni lazima
watafutwe na wachukuliwe hatua na
vyombo vya dola.
Mkuu Mkoa amesema kuwa kati ya
watumishi hewa 71 ni watumishi 34 hewa
wamefunguliwa mashitaka katika
mahakama mbalimbali kutokana kuchukua
fedha wasioifanyia kazi.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top