Madiwani ilala Dar watumbua jipu baada ufisadi kubainika.sima zaidi.
KAIMU MHANDISI MKUU WA KITENGO
CHA UJENZI MANISPAA YA ILALA
AWAJIBISHWA.
Kamati ya Fedha na Utawala ya Baraza la
Madiwani la Manispaa ya Ilala, Jijini Dar
es Salaam imemwajibisha Kaimu Mhandisi
Mkuu wa Kitengo cha Ujenzi wa Manispaa
ya Ilala Eng. Japhary Bwigane kutokana
na utendaji kazi mbovu.
Sanjari na hatua hiyo, watumishi wengine
wa kitengo hicho waliowajibishwa ni
Eng.Siyajali Mahili na Daniel Kirigiti
ambao ni wasaidi wa mkuu huyo.
Watumishi hao wote watatu
wanatuhumiwa kwa usimamizi mbovu wa
miradi mbalimbali chini ya kitengo hicho.
Kitengo hicho chini ya Eng. Bwigane
kimekuwa na utendaji kazi usioridhisha
kwa muda mrefu ikiwemo usimamizi
mbovu wa ujenzi wa barabara za
Manispaa ya Ilala hivyo kupelekea
kujengwa chini ya kiwango, miradi
kutokamilika kwa wakati ikiwemo daraja
la Bonyokwa kuchelewa kukamilika kwa
wakati.
Baadhi ya barabara zilizojengwa chini ya
kiwango ni Ukonga barabara ya Moshi
baa, tabata st. Mary's nk.
Uamuzi huo ulifikiwa na kamati ya fedha
na utawala kufuatia kikao kilichofanyika
tarehe 18/04/2016 siku ya jumatatu
katika ukumbi wa manispaa hiyo
Akizungumza na waandishi wa habari hii
leo ofisini kwake Mstahiki Meya wa
Manispaa ya Ilala mhe. Charles Kuyeko
CHADEMA/UKAWA juu ya uamuzi huo
alisema Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala
ameelekezwa kuendelea na taratibu za
kinidhamu juu ya watumishi hao ikiwemo
kushushwa vyeo.
Mstahiki Meya, mhe.Charles Kuyeko
ametumia fursa hiyo kuwaasa watumishi
wa Manispaa hiyo kutekeleza majukumu
yao kwa kufuata sheria, kanuni, taratibu
na miongozo ya utumishi wa umma, na
kuwaeleza kuwa hakuna atakayevumiliwa
kwa kutofuata sheria, kanuni, miongozo
na taratibu zilizowekwa.
Naye Naibu Meya, mhe. Kumbilamoto
akiongea katika mkutano huo na
waandishi wa Habari amewaasa watumishi
wa Manispaa hiyo wawe na moyo wa
kupenda kufanya kazi na wajitume katika
kutimiza majukumu yako kwa mujibu wa
taratibu za ajira zao.
Aidha mhe. Kuyeko amewahakikishia
wananchi wa Manispaa ya Ilala kuwa yeye
na baraza la madiwani ambalo
linaloongozwa na UKAWA watahakikikisha
Idara zote na vitengo vinafanyakazi kwa
ufanisi wa hali ya juu, Mtendaji yeyote
mbovu hatavumiliwa.
Imetolewa na;
Alex D. Massaba
Katibu wa Meya Manispaa ya Ilala, DSM.
0 comments :
Post a Comment