Benki ya dunia imeamua kuwasaidia wachimbaji wadogo wadogo wa madini hapa tanzania.soma zaid
Benki ya Dunia (WB) imeahidi kutoa Dola
za Marekani milioni 4 sawa na zaidi ya
shilingi Bilioni 8, kwa ajili ya Ruzuku
katika shughuli za uchimbaji mdogo wa
madini nchini.
Hayo yamebainishwa hivi karibuni jijini
Dar es Salaam na Waziri wa Nishati na
Madini, Profesa Sospeter Muhongo mara
baada ya kumaliza kikao na watendaji
Wakuu wa Benki ya Dunia wanaosimamia
Miradi ya Sekta ya Madini.
Profesa Muhongo alisema kuwa sehemu
ya fedha hizo za Ruzuku ambayo ni ya
Awamu ya Tatu zitatolewa mwezi
Septemba, 2016.
Aliongeza kuwa fedha hizo zitatumika
kufadhili uendelezaji wa vituo Saba vya
mfano vya utafutaji na uchimbaji mdogo
wa madini ambavyo vitachaguliwa na
Wizara baada ya kufanya tathmini ya
maeneo yanayoweza kuwekwa vituo
hivyo.
“Sio hivyo tu, Fedha hizi za Benki ya
Dunia zinalenga kuwafadhili wanawake
kwenye shughuli za uchimbaji mdogo wa
madini, ukataji na uchongaji wa madini ya
vito ili idadi ya wanawake
wanaojishughulisha na Sekta ya Madini
iongezeke,” alisema Profesa Muhongo.
Aidha, Profesa Muhongo alitoa wito kwa
wataalam wote wanaosimamia miradi
inayofadhiliwa na Benki ya Dunia katika
Sekta ya Madini kuhakikisha kuwa
utekelezaji wa miradi hiyo uende kwa kasi
ili kuleta matokeoyaliyotarajiwa.
Benki ya Dunia kupitia Wizara ya Nishati
na Madini imeendelea kutoa Ruzuku
katika Uchimbaji madini mdogo ambapo
katika mwaka wa Fedha 2015/16
zilitengwa takribani Shilingi bilioni 7.2
ambazo zilitolewa kwa vikundi 111 vya
wachimbaji wadogo na watoa huduma
mbalimbali katika sekta ya uchimbaji
madini mdogo.
Vilevile, katika mwaka wa Fedha
2013/2014, Fedha za Ruzuku zilizotolewa
kwa Wachimbaji Wadogo zilikuwa ni Dola
za Marekani 500,000 sawa na takribani
Shilingi Bilioni 1 zilizotolewa kwa
waombaji 11. Fedha hizi ziliwalenga
wachimbaji madini wadogo pekee tofauti
na awamu zilizofuata.
Utoaji huo wa Ruzuku unaenda
sambamba na utoaji wa elimu na mafunzo
kwa wachimbaji wadogo wa madini
waliopata ruzuku husika ili kuhakikisha
kuwa shughuli zilizopata ufadhili zinaleta
tija.
0 comments :
Post a Comment