Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, May 5, 2016

Mkuu wa mkoa wa singida amsimamisha mkurugenzi wa halmashauri ya singida kwa ufisadi.soma zaid.

Serikali mkoani Singida imemsimamisha kazi kwa
muda usio julikana Mkurugenzi wa halmashauri
ya wilaya ya Singida Bw. Simoni Mubee, baada
ya kutoa taarifa za uongo kuwa wafanyakazi
hewa kumina tisa hawajaisababishia hasara
serikali, huku uchunguzi umebaini kuwa shilingi
milioni mia moja ishirini na tano zimepotea.
Mkuu wa mkoa wa Singida Mhandisi Methew
Mtigumwe ametoa uamuzi huo mgumu kwenye
kikao cha maendeleo cha mkoa na kusema kuwa,
mkoa unafanya juhudi kuhakikisha fedha za
serikali hazipotei lakini kuna baadhi ya watumishi
wamekuwa wakificha takwimu kwa sababu ya
manufa yao wenyewe.
Katika hatua nyingine Mhandisi Mtigumwe
ametilia wasiwasi halmashauri ya wilaya ya
Singida miradi yake mingi inawezekana kujengwa
chini ya kiwango kwa sababu halmashauri hiyo
haina teknishani hata moja na ina mhandisi
mmoja ambaye ndiye anaye simamia miradi
yote,jambo ambao amesema atahakikisha
analifanyia kazi.
Kwaupande wake Kamanda wa Jeshi la polisi
Mkoani Singida ACP Thobiasi Sedoyeka kwa
kushirikiana na TAKUKURU mkoani Singida
wamesema, kutokana na agizo la mkuu wa mkoa
Jeshi lake litaendelea na uchunguzi ikiwemo
wafanyakazi wengine wa halmashauri hiyo na
endapo watabainika na makosa hatua kali zita
chukuliwa dhidi yao.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top