Ijue sababu iliyowafanya wabunge wanawake wa upinzani kutoka njee ya bunge leo Dodoma.
Wabunge wanawake wa Upinzani
wametoka wote nje ya Bunge kwa madai
ya kudhalilishwa bungeni na mbunge
mmoja wa CCM kuwa wanapewa viti hivyo
kwa kuwa na mahusiano na viongozi wao
wa juu.
Wabunge hao waliomba muongozo kwa
naibu spika lakini hawakusikilizwa ndipo
waliposimama wote na naibu spika
kuwataka kukaa chini na ndipo
kulipoibuka sekeseke la wabunge hao na
kuamua kususia kikao hicho cha bunge
asubuhi hii na kutoka nnje huku
wakiahidi kuja na tamko kali kuhusu
udhalilishaji waliofanyiwa huku naibu
spika tulia akifurahia tukio hilo
Msikilize hapa Mbunge wa Kawe na
Mwenyekiti wa Umoja Wanawake
CHADEMA, Halima Mdee akizungumza na
waandishi wa habari nje ya ukumbi wa
Bunge mjini Dodoma, baada ya wabunge
wanawake wa Ukawa kutoka nje ya
ukumbi wa Bunge kufuatia Mbunge wa viti
maalumu Sophia Mwakagenda kuomba
mwongozo wa Spika wa Bunge kwa kauli
aliyotoa jana Mbunge wa jimbo la Ulanga
Goodluck Mlinga kuzungumza bungeni
kuwa wabunge wa CHADEMA ili wapate
ubunge wa viti maalumu lazima wawe na
mahusiano na viongozi wao.
0 comments :
Post a Comment