Bidhaa za magendo zakamatwa na TRA mkoani kilimanjaro.som zaid.
Mamlaka ya mapato (TRA) mkoani Kilimanjaro
imekamata bidhaa kutoka nje za mamilioni ya
fedha baada ya kuvushwa kwa njia ya magendo
katika maeneo ya Kitobo, Kileo na Njiapanda
zikisafirishwa kwa njia ya magari mawili na
pikipiki tano.
Meneja wa TRA wa mkoa huo Bw. Abdul
Mapembe ameiambia ITV kuwa, katika
oparesheni hiyo ya kudumu wameyakamata
magari mawili moja likiwa na usajili wa kenya
likiwa na bidhaa hizo vikiwemo vifaa vya magari,
televisheni. Pikipiki, simu za mkononi, nguo,
mafuta ya taa, chumvi na sukari.
Bw.Mapembe amesema, wafanyabiashara wa
bidhaa hizo baada ya kukamatwa walitakiwa
wakalete vielelezo vya bidhaa zao kama
wamezilipia ushuru mpakani kama walivyodai
lakini hawajaonekana.
Kiongozi wa oparesheni hiyo Bw. Obednego
Nicholaus amewaonya wenye magari na pikipiki
hizo kuwa kama hawatajitokeza kulipia ushuru
bidhaa zitataifishwa pamoja na magari hayo aina
ya fuso na pikipiki.chanzo itv
0 comments :
Post a Comment