Bodi mpya ya .kupanga mishahara kuanza Agost2016.soma zaid.
BODI mpya ya kupanga mishahara kwa sekta
binafsi inatarajiwa kuanza kazi wakati wowote
kuanzia Agosti mwaka huu, baada ya bejeti kuu
ya serikali kupita.
Akizungumza na gazeti hili jana, Katibu Mkuu wa
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania
(Tucta), Nicholas Mgaya alisema, bodi hiyo
itakuwa na wajumbe 20 wakijumuisha wanne
kutoka kila eneo.
Alitaja maeneo hayo kuwa ni wawakilishi kutoka
serikalini, chama cha waajiri, vyama vya
wafanyakazi na wataalamu.
“Kila eneo litatoa wawakilishi wanne na sisi
wafanyakazi tayari tumeshapendekeza majina
yetu na maeneo mengine nayo yamekwisha
pendekeza majina”.
Alisema, kinachosubiriwa ni Waziri anayehusika
na Utumishi (Angella Kairuki) kutangaza kwenye
gazeti la Serikali ili bodi hiyo ianze kazi Agosti,
mwaka huu.
Bodi hiyo inaundwa baada ya serikali kufuta bodi
za kupanga mishahara za kisekta ambazo
zilionekana kutumia fedha nyingi kuziendesha.
Bodi hizo kwa mwaka jana zilitumia Sh mil 450
kuziendesha.
“Hili wazo la kuundwa kwa bodi mbili tu yaani ya
sekta binafsi itakayojumuisha sekta 12 za binafsi
na bodi ya kupanga mishahara ya sekta ya umma
ilitolewa na serikali nasi wafanyakazi
tukakubaliana nalo. Sasa hivi kilichobaki ni
kuundwa kwa bodi ya kupanga mishahara ya
utumishi wa umma,” alisema.
Alisema licha ya kutofahamu kima kipya cha
chini ya mshahara kwa watumishi wa serikali
ambacho kinatarajiwa kutangazwa wakati waziri
anayeshughulikia utumishi atakapotangaza, Tucta
wanasisitiza kupata kima cha chini sekta zote
kiwe Sh 750,000 bila kukatwa kodi.chanzo habar leo.
0 comments :
Post a Comment