Ijue idadi ya wanafunzi wanaokufa kwa ajali za barabarani kila mwaka hii ni kwa mjibu wa takwimu iliyotolewa.soma zaid.
Jeshi la polisi nchini limesema wanafunzi 78
nchini wamepoteza maisha kutokana na ajali za
barabara huku 181 wakijeruhiwa katika kipindi
cha mwaka 2015.
By Hadija Jumanne, Mwananchi hjumanne@
mwananchi.co.tz
Dar Es Salam. Jeshi la polisi nchini limesema
wanafunzi 78 nchini wamepoteza maisha
kutokana na ajali za barabara huku 181
wakijeruhiwa katika kipindi cha mwaka 2015.
Hayo aliyasema leo na Mnadhimu wa Kikosi cha
Usalama barabarani kutoka Makao Makuu,
Fortunatus Muslim wakati wa utoaji zawadi kwa
washindi wa shindano la uchoraji alama za
usalama barabarani.
Muslim alisema kati ya wanafunzi 78 waliofariki,
wavulana walikuwa 40 na wasichana 38, huku
majeruhi wakiwa 181 ambapo kati ya hao
wavulana walikuwa 81 na wa kike 81.
"Maeneo hatarishi ambayo yanaongoza kwa
kusababisha ajali za barabarani katika Jiji la Dar
Es Salaam ni Lumumba, Mnazi mmoja, Mikumi,
Mtambani, Boko, Bunju na Kongowe." Alisema
Muslim.
Mashindano hayo ambayo yaliandaliwa na
kampuni ya Puma Energy yalilenga kutoa elimu
kwa wanafunzi wa shule za msingi juu ya
utumiaji wa alama za usalama barabarani.
"Jeshi la Polisi kupitia kikosi cha usalama
barabarani limeendelea kutoa elimu kwa
wanafunzi, madereva na Jamii kwa ujumla juu ya
matumizi sahihi ya barabarani" aliongeza Muslim
Alisema wanafunzi walioshinda shindano la
uchoraji wa alama za usalama barabarani ni
Shaibu Abdalah kutoka shule ya msingi Gongo la
mboto, Abdallah Hussein kutoka Osterybay na
Christian Mathias kutoka Gongo la mboto.
Awali, Meneja wa kampuni ya Puma Enegy,
Philippe Corsaletti alisema lengo la mashindano
hayo ni kutoa elimu kwa wanafunzi kuhusiana na
matumizi sahihi ya barabarani.chanzo mwananch.
0 comments :
Post a Comment