Maafisa elimu wa halmashauri sita mkoan mara wasimamishwa kazi .soma zaid.
Mkuu wa mkoa wa Mara Bw.Magesa Mulongo
ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa
maafisa elimu wa halmashauri sita za mkoa wa
Mara huku Wakurugenzi Watendaji wa
halmashauri hizo wakitakiwa kujieleza baada ya
kushindwa kutoa zawadi za watumishi bora wa
idara ya elimu kwa mwaka mmoja hadi miwili
hatua ambayo amesema inachangia kushusha ari
ya utendaji wa kazi kwa watumishi hao.
Mkuu huyo wa mkoa wa Mara Bw.Magesa
Mulongo,ametoa agizo hilo mjini Musoma katika
viwanja vya shule ya msingi ya Mkendo wakati
wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani
katika mkoa wa Mara na kuelezwa na baadhi ya
viongozi wa vyama vya wafanyakazi katika wilaya
hizo kuwa licha kuteuliwa kwa wafanyakazi bora
lakini halmashauri hizo katika kipindi cha mwaka
jana na mwaka huu zimeshindwa kutoa zawadi
kwa wateule wao.
Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa vyama
vya wafanyakazi mkoani Mara wakizungumza
katika maadhimisho hao mbali na kulaani vitendo
vya unyanyasaji vinavyofanywa na baadhi ya
waajiri dhidi ya watumishi lakini pia wamelaani
vikali kitendo cha waajiri kuwakata fedha
watumishi wao kwa ajili ya kununulia
vitambulisho vya kazi.
Awali wafanyakazi hao wa idara mbali za serikali
na sekta binafsi mkoani Mara wamefanya
maandamano wakiwa na mabango yenye ujumbe
mbalimbali yakianzia uwanja wa Posta hadi
uwanja wa mkendo huku mkuu huyo wa mkuu wa
Mara akitumia nafasi hiyo pia kuwataka waajiri
wote kuanzia sasa kutenga kiasi cha fedha kama
zawadi kwa kila mfanyakazi bora anayeteuliwa
kutoka katika idara yake.chanzo itv.
0 comments :
Post a Comment