Breaking News
Loading...

Advert

Saturday, April 30, 2016

Tatizo la maji Dar limekuwa kero, serikali kuondoa kero hizo.soma zaid.

Serikali ya Tanzania imewahakikishia wakaazi
wa jiji la Dar es Salaam kwamba inatatua tatizo
la uhaba wa maji mjini humo na hivi karibuni
tatizo hilo litakuwa historia.
Kulingana na gazeti la The Citizen nchini
Tanzania,naibu waziri wa maji na unyunyizaji Bw
Issack Kamwelwe amesema kuwa serikali kwa
sasa imeanzisha mradi wa kuimarisha
usambazaji wa maji katika maeneo ya mji
yanayokumbwa na uhaba mkubwa wa maji.
Kulingana na Bw Kamwele,mradi huo ambao una
thamani ya dola milioni 32.9 na na unaotarajiwa
kukamilika mwezi Aprili mwaka 2017
unashirikisha kubadilisha mabomba ya zamani,na
kuweka mapya na kuweka mabomba mapya
maeneo ambayo hayajaangaziwa.
Baadhi ya maeneo ambayo yatafaidika na mradi
huo ni mji wa
bagamoyo,Mpiji,Bunju,Mabwepande,Boko,Bweni,Te
geta,Ununio,Wazo,Salasala, Kizundi,matosa,Mbezi
juu,Goba,Changabyikeni,makongo,Kiluvya,Kibamba,
Mbezi,Msakuzi,Mkabe,Maramba Mawili na
Msigali.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top