Leo ni siku ya maadhimisho ya uhuru wa habari wewe mdau unalipi la kuongeo juu ya uhuru wa habar.
Leo ni siku ya Madhimisho wa Uhuru wa
Habari, maadhimisho ya Mwaka Huu
yanafanyika kitaifa mjini Mwanza, Waziri Nape
Mnauye, Mzee Reginald Mengi, Baraza la
Habari Tanzania, MCT, Tanzania Media
Foundation, TMF, Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania, TCRA, MISA TAN,
Shirika la Umoja wa Mataifa UN ... na
wengine wengi wako ndani ya nyumba.
Maadhimisho yameishaanza asubuhi hii,
andamana nami nikikuletea kile
kinachojiri, ila kama kuna mwana JF
mwingine, tusaidiane ku update.
Karibu.
Paskali.
=====
Anyazungumza sasa ni Pili Mtambalike
anawakilisha Baraza la Habari Tanzania,
Media Council of Tanzania, MCT,
ameikumbushia kauli mbia ya
maadhimisho haya kwa mwaka huu,
"Kupata habari ni haki yako, idai!"
===
Sasa hivi anazungumza Edda Sanga,
Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa
Habari Wanawake Tanzania, TAMWA.
===
Sasa anazungumza Mwenyekiti wa Chama
cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari,
MOAT, Dr. Reginald Mengi.
Mengi amekemea rushwa kwenye vyombo
vya habari, amesema zile bahasha ni
rushwa, hivyo wapokea bahasha ni
majipu!, watumbuliwe!.
Duu!.
===
Leo Tumemkumbuka Mwangosi!.
Tumesimama dakika moja for him.
======
Waziri Nape
Wanahabari fichueni maovu bila woga na
mtukosoe ili tuijenge Tanzania yetu kwa
pamoja!
Sote ni watanzania, tunaweza kukaa na
kuamua kwa pamoja kuhusu hili la Bunge
Live
Tunaweza kukaa mezani kuamua upya
kuona namna bora ya kuboresha suala
urushaji wa matangazo ya Bunge
Uamuzi wa kuanzisha studio ya Bunge ni
uamuzi uliopitishwa na Bunge lililopita
kabla hata sijawa mbunge
Tutatunga Sheria kwa kuzingatia Sera
iliyopo. Muswada ukipita, utafuta sheria
kandamizi kama ile ya 1976
Maoni ya wadau juu ya maboresho ya
Muswada wa Vyombo vya Habari
yatafanyiwa kazi. Tunatunga sheria kwa
ajili ya watu
Kuna sheria zinalalamikiwa kuwa na
mapungufu... Serikali itakaa chini
kuangalia namna ya kuzirekebisha!
Nawahakikishia, Tutalinda, kuutetea na
kuukuza Uhuru wa Vyombo vya Habari
Tanzania
Z
0 comments :
Post a Comment