Sumaye aibuka na kusema maneno haya dhidi ya Rais maguful.soma zaid
FREDERICK Sumaye, Waziri Mkuu Mstaafu
ameeleza kushangazwa na Serikali ya Rais John
Magufuli kupenda kusifiwa zaidi na kuchukia
kukosolewa,
Sumaye bila kumtaja jina Rais Magufuli
ameleza kushangazwa na hatua ya serikali
kuminya uhuru wa habari na kwamba,
kufanya hivyo kunalenga kuficha madudu
yanayofanywa na watendaji wake.
“Wapowatawala ambao hawapendi kusemwa
lakini wanapenda sana kusifiwa. Kiongozi
mwenye tabia ya udikteta hataki kusikia kingine
zaidi ya sifa zake tu.
“Huyo ni mtu hatari na katika nchi ya namna hiyo
hakuna uhuru wa habari wala uhuru wa kutoa
maoni kwa woga wa kupotezwa kusikojulikana,”
amesema Sumaye.
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini
Dar es Salaam katika maadhimisho ya Siku ya
Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyoratibiwa na
Chama cha Waandishi wa Habri za Siasa
(TAPOREA), Sumaye amesema, serikali inakiuka
Katiba ya nchi.
Amesema, serikali yoyote inayopambana na
vyombo vya habari na kuminya uhuru wa kufanya
kazi zao huwa ina tatizo kwa upande wa
wanaotawala.
Akitolea mfano wa hatua ya serikali kuzuia
matangazo ya moja kwa moja ya bunge Sumaye
amesema, kwa kufanya hivyo serikali imevunja
Katiba.
“Unapoondoa matangazo ya moja kwa moja ya
vipindi vya Bunge, kwanza ni kuvunja katiba.
Ibara ya 18 (d) ya Katiba inasema, kila mtu ana
haki ya kupewa taarifa wakati wote.
“Kwa kuzuia Bunge kuoneshwa ‘live’ (moja kwa
moja) wewe serikali unataka kutoa taarifa ya
Bunge kwa wakati unaoutaka na kwa taarifa
unayoitaka wewe,” ameeleza Sumaye.
Kuhusu sababu iliyotolewa kwamba, matangazo
hayo yanatumia gharama ya Sh. 4 bilioni
amesema haina mashiko.
Sumaye amesema, hata kama matangazo hayo
yatarushwa na ofisi za bunge bado, gharama
zitaongezeka zaidi kwa sababu Bunge litahitaji
kununua mitambo pamoja na kuajiri wafanyakazi
wake.
Sumaye amesema, serikali yenye demokrasia ya
kweli lazima ikubali wananchi wake kutoa maoni.
“Serikali yoyote yenye utawala bora, ingependa
mambo yake inayoyafanya kwa ajili ya wananchi
wake mambo hayo yajulikane kwa wananchi hao.
“Ukiona serikali inaficha mambo yake lazima
kuna mambo wanayoyafanya ambayo hayafai na
wasingependa jamii ijue,” amesema Sumaye.
George Maziku, Mkurugenzi Mtendaji wa
TAPOREA amesema, ripoti ya hali ya uhuru wa
waandishi wa habari na uhuru wa vyombo vya
habari kimataifa, iliyotolewa na Shirika la
Waandishi wa Habari Wasio na Mipaka lenye
Makao Makuu yake nchini Ufaransa haipendezi.
Amesema, ripoti hiyo inaonesha kuwa, katika
miaka 10 iliyopita zaidi ya waandishi wa habari
800 kutoka mataifa mabalimbali duniani
wameuawa wakiwa wanatekeleza kazi zao.
“Kitisho kingine kwa uhuru wa vyombo vya habari
nchini ni utamaduni mpya ulioasisiwa na
kuimarishwa na watawala wa sasa na
kuvishinikiza vyombo vya habri kutomkosoa Rais
John Magufuli na serikali yake.
“Matokeo yake, vyombo vingi vya habari nchini
vimelazimika kuandika habari za kumfurahisha
Rais Magufuli,” amesema Maziku.chanzo mwanahalisonline
0 comments :
Post a Comment