Wanafunzi wa shule za msingi kenya waanza kunufaika na kompyuta.soma zaid.
Wanafunzi wa darasa la kwanza katika shule za
msingi, 151, nchini Kenya wamepokea kompyuta
hizo siku ya Jumanne.
Usambazaji wa tablets hizo unahusisha
wanafunzi 11,570 wa darasa la kwanza katika
shule 151 zilizoteuliwa.
Katika kaunti ya Mombasa, wanafunzi wa shule
ya Upili ya Sparki wamekabidhiwa kompyuta hizo.
"Tumepokea 'tablets' 80, laptopu mbili
zitakazotumiwa na walimu pamoja na mashine
moja ya kifaa cha kuonyesha picha kwenye ukuta
kwa kutumia mwanga". Anasema mwalimu mkuu
wa shule ya msingi ya Sparki Alfred Nthiga.
'Tablets' hizo zinawawezesha kutafuta maelezo
kwenye mtandao wa 'google'.
Katika mkondo wa kwanza wa kutekeleza mradi
huo, takriban shule tatu katika kila kaunti,
wanafunzi watopokea 'tablets', huku walimu
wakikabidhiwa laptopu
Kila shule iliyoteuliwa kupata vifaa hivyo kote
nchini itawezeshwa kupata huduma za mitandao
kwa kutumia Wi-Fi.
Mradi huo utaigharimu serikali ya Kenya dola
milioni 170.
Mradi huo wa kuwapa wanafunzi wa darasa la
kwanza tarakilishi bila malipo ni miongoni mwa
ahadi kuu za uchaguzi ambazo serikali tawala ya
Jubilee ilitoa mwaka wa 2013.
Hata hivyo utekelezwaji wa mradi huu
umekwazwa na tetesi za ufisadi pamoja na kesi
nyingi mahakamani.
Ahadi ya serikali ya Jubilee ya kutoa laptopu kwa
kila mwanafunzi wa darasa la kwanza katika siku
100 za kwanza haikutimizwa na badala yake,
laptopu zikabadilishwa na vibao vya 'tablets'
Serikali ya Jubilee pia iliahidi kuwapa wanafunzi
wa shule za msingi maziwa bila malipo, ahadi
ambayo hadi sasa haijatimizwa.
Baadhi ya wakosoaji wanashikilia kuwa mradi huo
haufai kupewa kipau mbele ikizingatiwa matatizo
chungu nzima yanayoikumba sekta ya elimu;
ikiwemo migomo ya walimu wakidai nyongeza ya
mishahara na ukosefu wa nguvu za umeme
katika maeneo mengi ya mashinani nchini Kenya.
0 comments :
Post a Comment