Majambazi wanne wameuwawa mkoani tanga.
Watu wanne wanaosadikiwa kuwa majambazi
ambao wanadaiwa kuhusika katika matukio
mawili tofauti ya uhalifu ikiwemo kuua watu
watano kisha kupora fedha katika duka la bidhaa
mbalimbali jijini Tanga wameuawa na Polisi
katika majibizano ya risasi baina yao katika
Mapango ya amboni yaliyopo nje kidogo mwa jiji
hilo.
Kamanda wa Polisi mkoani Tanga Kamishna
Msaidizi wa Polisi nchini Leonard Paul amesema
jijini Tanga kuwa baada ya kuuawa majambazi
hayo yalikutwa yakiwa na silaha mbali mbali
ikiwemo risasi za silaha aina ya Shotgun
zipatazo 120 kofia maalum za kuvalia usoni
wakati wa uhalifu na silaha nyingi baridi
wanazotumia wakati wa uporaji.
Kamanda Paul amesema katika tukio la
majibizano ya risasi askari wawili waliojulikana
kwa majina ya PC Charles alipigwa bomu katika
Mapango ya Amboni na kujeruhiwa sehemu za
mwili wake pamoja na Inspekta Mwakisol
ambaye risasi ilimparasa sehemu za usoni wakati
walipokuwa wakijibizana kwa risasi.
Kufuatia hatua hiyo Mbunge wa jimbo la Tanga
Mussa Mbaruk amesifu jitihada za jeshi hilo na
kulitaka kuongeza jitihada za kuimarisha hali ya
amani na utulivu kwa sababu jiji la Tanga
linatarajiwa kupokea sehemu kubwa ya
wawekezaji kutoka nje ya nchi ambao
wamevutiwa na fursa zilizopo kwa ajili ya
kuwekeza katika sekta ya viwanda.chanzo itv
0 comments :
Post a Comment