Tatehe 05 mei 2016 ACT-WAZALENDO kuazimisha miaka miwil ya kuzaliwa kwake.nini maoni yako.
ACT-WAZALENDO kuadhimisha miaka miwili ya
kuzaliwa kwake Alhamis wiki hii Mkuranga
,Pwani.
Tarehe 05 Mei, 2016 Chama cha ACT Wazalendo
kitaadhimisha miaka miwili ya kuzaliwa kwake.
Kitaifa, maadhimisho haya yatafanyika wilayani
Mkuranga mkoa wa Pwani mgeni rasmi katika
maadhimisho haya atakuwa Mwenyekiti wa
Chama Taifa Mama Anna Mghwira.
Mwenyekiti wa Taifa Mama Anna Mghwira
ataambatana na Kaimu Katibu Mkuu Ndugu
Juma Sanani pamoja na viongozi wengine wa
kitaifa.
Katika maadhimisho hayo Mwenyekiti wa Chama
Taifa atazindua matawi mapya zaidi ya ishirini,
kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii na
baadaye kuhutubia mkutano wa hadhara
Mkuranga Mjini.
Kwa upande wa Zanzibar, Maadhimisho haya
yataenda pamoja na wanachama na viongozi wa
ACT Wazalendo kujitolea damu kwenye Benki ya
Damu Zanzibar na kutoa misaada mbalimbali
kwenye kituo cha Wazee cha Barazani “Barazani
kwa Wazee”.
Kwa sasa shamra shamra za maadhimisho haya
yanafanyika pia kwenye mikoa yote nchini kwa
viongozi na wanachama wa ACT-Wazalendo
kushiriki katika shughuli za kijamii kabla ya siku
ya hitimisho yake Alhamis Mei 5.
Abdallah Khamis,
Afisa Habari
ACT Wazalendo
Imetolewa leo tarehe 03 Mei, 2016
0 comments :
Post a Comment