Breaking News
Loading...

Advert

Tuesday, May 3, 2016

IMF, uchumi wa Tanzania unatalajia kukua kwa 6.9% mwaka huu 2016.soama zaid.

Tanzania inatarajiwa kusajili kiwango cha juu
zaidi cha ukuaji wa uchumi wake mwaka huu
katika kanda ya Afrika Mashariki na kati.
Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la fedha la
kimataifa - IMF.
Katika ripoti yake iliyotolewa hii leo Tanzania
inatarajiwa kusajili kiwango cha juu cha ukuaji
wa uchumi wake wa asilimia 6.9% mwaka wa
2016.
Kasi hiyo ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania ni ya
pili tu nyuma ya Ivory Coast baina ya mataifa ya
Kusini mwa jangwa la Sahara .
Ivory Coast inatarajiwa kukuwa kwa kasi ya
asilimia 8.5%.
Katika kanda ya Afrika Mashariki ,uchumi wa
Kenya ndio wa pili kwa kasi ya ukuaji kwa
asilimia 6%.
IMF hata hivyo inasema kuwa kasi ya ukuaji wa
uchumi kusini mwa jangwa la Sahara unatarajiwa
kupungua kwa mwaka wa pili mfululizo kutokana
na kudorora kwa viwango vya uzalishaji na hivyo
uwekezaji.
Kwa mujibu wa shirika la fedha la kimataifa -
IMF, eneo hilo linakadiria kushuka kwa ukuwaji
wa uchumi kwa asilimia 3 mwaka huu.
Kiwango hicho ni cha chini kabisa kuwahi
kushuhudiwa katika miaka 15.
Mataifa yanayotegemea mapato yanayotokana
na mafuta ndiyo yalioathirika zaidi kama vile
Nigeria na Angola.
Aidha Zambia pia imeathirika vibaya kutokana na
ukosefu wa soko la kimataifa la shaba yake.
Ripoti hiyo inaitaja Afrika Kusini kama moja ya
mataifa ambayo kiwango chake cha ukuaji
kimedorora kwa kiasi kikubwa mno.
Katika orodha ya mataifa yanayotarajiwa kuwa
na kiwango cha juu cha ukuaji Kusini mwa
jangwa la sahara Ivory Coast ndio inayoongoza.
Orodha ya mataifa ya kanda ya Kusini mwa
Jangwa la Sahara na viwango vya kasi ya ukuaji
wa uchumi 2016.
1. Ivory Coast 8.5%
2. Tanzania 6.9%
3. Senegal 6.6%
4. Kenya 6%
5. Zambia 3.4%
6. Nigeria 2.3%
7. Afrika Kusini 0.6%

0 comments :

Post a Comment

Back To Top