Makandarasi 4000 hapa nchini wafutiwa leseni za usajili kampuni za ukandarasi.
Bodi ya usajili wa Makandarasi nchini imezifutia
leseni za usajili kampuni za ukandarasi zaidi ya
4000 kati ya kampuni 12000 za kizalendo baada
ya kubaini hazinauwezo wa kutekeleza miradi ya
maendeleo ya jamii ili kunusuru upotevu wa
fedha za umma.
Kaimu msajili wa bodi ya usajili wa Makandarasi
nchini Bw.Rhoben Nkori amebainisha hayo jijini
Mwanza wakati akizungumza na ITV baada ya
mkutano mkuu wa bodi ya Makandarasi uliolenga
kuwajengea uwezo makandarasi kanda ya ziwa
amesema hatua ya kuwafutia usajili baadhi ya
wakandarasi imetokana na kushindwa kutimiza
vigezo vinavyotakiwa ikiwemo ukosefu wa
vitendea kazi vinavyositahili.
Kutokana na ukosefu wa vitendea kazi kwa
wakandarasi wazalendo baadhi ya kampuni za
uwekezaji kutoka nje ya nchi zimejitokeza kuunga
mkono juhudi za serikali ikiwemo kampuni
inayokopesha vifaa vya ujenzi kwa makandarasi
na halmashauri za wilaya hapa nchini Lantrack
Tanzania Company Limited ambayo inatoa
mikopo ya vifaa kwa makanda rasi wazalendo
bila liba yoyote.
Hatua hiyo imetokana na tishio la waziri wa
ujenzi uchukuzi na mawasiliano Prof. Makame
Mbawara siku moja wakati alipotangaza kuifuta
bodi ya usajiri wa Makandarasi endapo
itashindwa kusimamia utendaji kazi wa viwango
vinavyotakiwa kwa wakadarasi hapa nchini.
0 comments :
Post a Comment