Serikal haitowavumilia viongozi na watumishi wa umma wanao jihusisha na ufisadi na rushwa nani kasema soma zaid.
Rais Magufuli amerejea kauli yake kuwa serikali
yake haitawavumilia viongozi na watumishi wa
umma ambao wamekuwa wakijihusisha na
vitendo vya rushwa na ufisadi, huku akisema
ataendelea kutumbua majipu kwa yeyote
atakayebainika kuchezea mali za umma ili
kulinda maslai ya wengi, hususani watanzania
wanyonge.
"Ninafanya kwa niaba yenu, ninafanya kwa niaba
yenu, ningekuwa sifanyi kwa niaba yenu, na mimi
ningeingia madarakani ningeanza kushirikiana na
hao, na wengine walifikiria nitashirikiana nao,
wamekwama mimi nitawatumbua kila siku ili
Tanzania iwe ya neema iweze kwenda mbele,
haiwezekani nchi kama hii tajiri, Tanzanite ipo,
dhahabu ipo, wanyama mpaka nyani wameanza
kuuzwa, wakimalizika nyani si tutauzwa na sisi
ndugu zangu, ni lazima nisimamie hili"
amesisitiza Dkt. Magufuli.
Aidha katika mazungumzo hayo, Rais Magufuli
amewahakikishia kuwa serikali yake imeanza
kuwashughulikia wafanyabiashara ambao
wameficha sukari kwa makusudi na kusababisha
upungufu wa bidhaa hiyo.
Rais Magufuli amesema tayari vyombo vya dola
vimekamata tani 5,000 za sukari iliyofichwa na
mfanyabiashara mmoja huko Tabata Jijini Dar es
salaam na pia vimembaini mfanyabiashara
mwingine aliyeficha sukari hiyo Jijini Arusha.
"Kweli nitawakomesha hawa, wasije
wakanilaumu, haiwezekani ukaficha sukari wakati
viwanda vyetu vinatengeneza sukari, kuna mmoja
mwingine yupo Arusha hapa, nae ameficha
sukari, alienda akanunua kwenye viwanda vya
sukari vya hapa akaificha yote, leo
ninamshughulikia.
"Kuna mwingine alinunua sukari pale Kilombero
zaidi ya tani 3,000 akaficha, na mwingine
ameshikwa pale Tabata alikuwa ameficha tani
5,000, na wanasubiri katika mwezi Mtukufu wa
Ramadhani ili ndugu zetu Waislamu wapate
shida, haya ni mashetani makubwa, unawafichia
watu chakula ambacho wanatakiwa kula, lakini
nataka niwahakikishie ndugu zangu, hili ni tatizo
la muda Tanzania, sukari itapatikana kwa wingi,
na itanunuliwa na serikali, tumeshaagiza sukari
lakini hatutawapa vibali hawa wafanyabiashara
ambao wanatunyonya, tutanunua wenyewe na
tutauza bei ya chini, hilo ndio lengo la serikali"
Amesema Rais Magufuli
0 comments :
Post a Comment