DC akabidhiwa ushahidi wa kupigwa mwalimu mkoan katavi wilayani sumbawanga.soma zaid.
CHAMA cha Walimu (CWT) Rukwa, kimemkabidhi
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Mathew
Sedoyeka ushahidi wa maandishi unaoelezea
kitendo cha Ofisa Elimu, Shule za Msingi katika
Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, Peter
Fusi, kumshambulia na kumpiga makofi mwalimu
mwenzao akiwa darasani.
Ushahidi huo ulikabidhiwa kwa Mkuu wa wilaya
na Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Rukwa, Hance
Mwasajone.
Ushahidi huo wa kimaandishi wa tukio hilo
umeandikwa na mwalimu mwenyewe, Jacob
Msengezi (25) ambaye alisema alipigwa mbele
ya wanafunzi wake akiwa darasani shule ya
msingi Kianda kabla ya kuamuru walimu wengine
kufanya usafi kwa kuokota mbigili ‘miba’
iliyotapakaa katika eneo la shule hiyo akidai
kuwa huo ni uchafu.
Sedoyeka aliwaruhusu viongozi hao kumtembelea
mwalimu na kusisitiza kuwa anafuatilia kwa
karibu mkasa huo ili sheria ichukue mkondo wake.
0 comments :
Post a Comment