Meya wa jiji la Dar es salaam leo amepata ugeni kutoka kampuni ya KOYO ya japani.
Meya wa Jiji la Dar es salaam Mstahiki # Isaya
Mwita leo amepata ugeni kutoka nchini Japan.
Ametembelewa na ujumbe wa watu watano
kutoka kampuni ya KOYO ya Japan wakiongozwa
na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw.
Norio Shoji.
Ujumbe huo umrfika ofisini kwa mstahiki meya
kufanya mazungumzo na kuangalia namna ya
kushirikiana na Halmashauri ya jiji la Dsm katika
miradi ya kijamii, ikiwemo usafi wa Jiji la Dar es
salaam, huduma ya maji na umeme katika taasisi
kama vile shule, zahanati, nk. Aidha ujumbe huu
ulifanya mazungumzo kuhusu uwekezaji katika
sekta ya uchumi katika jiji la Dar es salaam.
Utekelezaji wa mipango iliyozungumzwa hasa ya
kijamii itahusianishwa na program zinazoendelea
kutekelezwa na shirika la JICA kutoka Japan.
0 comments :
Post a Comment